![]() |
Nexus 5 |
Hapo jana, mmoja wa wasemaji wa kampuni ya Google alitoa taarifa kwamba utengenezaji wa smartphone hii umefikia mwisho kabisa na kuongeza kwamba hazitarudi sokoni, akisema "once they are gone, they are gone". Kauli hii imechanganya watu wengi sana hasa wale walio wapenzi wa devices za Nexus. Lakini, kauli nyingine imetolewa ikidai ya kwamba utengenezaji kwa sasa umesimama na mauzo ya smartphone hii yatarudi tena
mwakani kuanzia kipindi cha mwezi wa kwanza hadi wa tatu(Quarter One) katika wauzaji wachache tu watakaoidhinishwa na Google Play Store ikiwa moja ya wauzaji. Baada ya muda huo hatutaiona smartphone hii sokoni.
mwakani kuanzia kipindi cha mwezi wa kwanza hadi wa tatu(Quarter One) katika wauzaji wachache tu watakaoidhinishwa na Google Play Store ikiwa moja ya wauzaji. Baada ya muda huo hatutaiona smartphone hii sokoni.
Pamoja na kwamba kuna nafasi nyingine ya kujipatia smartphone hii. Nina wasiwasi kusema kwamba, hali haitakuwa sawa na ilivyo sasa. Muda huo smartphone hii itakuwa na gharama sana na ukilinganisha na bei inayouzwa kwa sasa. Itakuwa haina maana kwa sababu moja ya sifa ya devices za Nexus ni kwamba bei yake huwa ni nafuu huku zikiwa specifications za hali ya juu ukilinganisha na devices nyingine. Ukomo huu wa utengenezaji unatokana na kuja kwa smartphone nyingine ambayo ni kaka wa Nexus 5 inayofahamika kama Google's Nexus 6. Hii ikiwa imetengenezwa kwa ushirikiano wa Google na kampuni ya Motorola Mobility ambayo kwa sasa ipo chini ya kampuni ya Lenovo.
No comments :
Post a Comment