Dec 11, 2014

"Oppo Find 7", smartphone iliyo na camera yenye 50MP(Mega Pixels).

Oppo Find 7
Oppo electronics, kampuni ya kichina inayojihusisha na utengenezaji wa vifaa vya kielectroniki(consumer electronics). Kwa walio wengi, hili ni jina geni kidogo na kwa sababu ni kampuni ya kichina isije kukupelekea kuwaza kwamba wanatengeneza bidhaa zenye ubora mdogo na zilizo feki. Bidhaa nyingi za kampuni hii soko lake lipo China, Ulaya na Marekani, nadhani unaelewa
 wazi kabisa kampuni linahitaji viwango gani vya ubora ili kupata mpenyo wa kibiashara nchini Marekani.
Hutakiwi kuwa na wasiwasi na brand hii!


Mnamo mwezi wa tano mwaka huu, walizindua smartphone yao inayofahamika kama Oppo Find 7.
Kilichowavutia watu wengi kuhusu smartphone hiyo ni kuwa na display
ambayo ni UltraHD 2K(aina ya display ambayo ina ubora mara mbili ukilinganisha display ya FullHD, Full HD zina horizontal pixels kiasi cha 1080pixels, UltraHD 2K zina 2048pixels=2K na UltraHD 4K zina ubora mara nne wa FullHD), display hii ikiwa na pixel density kubwa mno yenye kufanya muonekano wa display kuwa wa kiwango cha hali ya juu mno, 538ppi(pixels per inch), smartphone kama Samsung Galaxy S5 ina 432ppi tu.

Mshangao na hamaki kubwa ni pale Oppo alipotangaza kwamba Find 7 ina kamera yenye uwezo wa 50 Megapixels!. Ukweli ni kwamba, smartphone hii haina kamera ya sensor yenye uwezo wa 50 megapixels. Kilichofanyika hapa ni ujanja wa kiprogramu "software trick", kamera iliyopo katika Find 7 imetengenezwa na kampuni ya Sony ikiwa na uwezo wa 13 megapixels tu ikiwa na dual-LED flash pia. Ili kupata picha ya 50 megapixels, smartphone hii inakuja na feature ya software inayoitwa "super zoom", super zoom inafanya kaujanja haka "unapopiga picha, camera itapiga picha 10 kwa wakati mmoja bila hata ya wewe kutambua na itachagua 4 zilizo bora kati ya hizo 10, baada ya hapo itafanya image recombination na kupata picha yenye 50MP", mchakato(process) nzima inatokea kwa sekunde na hautagundua yote haya yanavyofanyika kwa sababu ni well automated process, mwisho wa siku utapata picha bora ambayo utaizoom mara nyingi bila kuharibika(blurred) ikiwa na 50MP resolution!

No comments :

Post a Comment