Miaka 11 iliyopita Nokia alizindua smartphone hii, enzi hizo Nokia 6600 ilikuwa ndiyo smartphone yenye kutumia teknolojia ya hali ya juu katika smartphones zote za Nokia zilizowahi kutengenezwa kabla. Ikiwa na camera, TFT(Thin Film Transistor) display yenye uwezo wa rangi 65,000(65k), uwezo wa kucheza muziki na display yenye muonekano wenye kiwango cha hali ya juu. Smartphone nyingi zilizokuwepo kipindi hicho hazikuwa na uwezo kama huu. Ili kuweza kuimiliki smartphone hii kwa muda huo ilibidi uwe na shilingi za kitanzania zipatazo laki tisa, unaweza fikiria kwa mwaka 2003 shilingi laki tisa ilikuwa na thamani kiasi gani kulinganisha na thamani ya pesa kwa sasa.
![]() |
Nokia 6600 |
Miaka hiyo hakukuwepo smartphone zenye processors kama zilizopo sasa mfano. dual core processors(CPU mbili), quad core processor(CPU nne) n.k ambazo nyingi ya hizi huwa na spidi inayoanzia 1.5GHz(Giga-Hertz) na kuendelea kwa kila CPU. Single core(CPU moja) processor ndizo zilikuwa zikitumika, Nokia 6600 ikiwa na processor ya single core yenye spidi(clock speed) ya 104MHz(Mega-Hertz), ni processor yenye spidi ndogo sana ukilinganisha na teknolojia tuliyonayo sasa, lakini kwa muda huo processor hii ilikuwa ikionekana yenye
spidi maradufu. Ni kama leo hii tuionavyo smartphone kama HTC M8 ilivyo na kasi kubwa katika kuchakata data ikiwa na processor yenye spidi ya 2.3GHz(quad core).
spidi maradufu. Ni kama leo hii tuionavyo smartphone kama HTC M8 ilivyo na kasi kubwa katika kuchakata data ikiwa na processor yenye spidi ya 2.3GHz(quad core).
Sahau habari ya "selfies" enzi hizo maana hakukuwa na smartphone yoyote yenye camera ya mbele(front facing/secondary camera) na Nokia 6600 ni moja ya smartphones za mapema kuwa na camera ya nyuma(primary camera) ya VGA[640X480pixels](Vertical Graphics Array) ikiwa na 0.3 megapixels, inafurahisha kidogo! Siku hizi camera nyingi za smartphones zina sensors zenye uwezo wa 8 megapixels hadi kufikia 21 megapixels. Muda huo kamera ya 0.3MP ni bonge la mafanikio kwa mtengeneza smartphone na hata katika matangazo swala la kutaja megapixel ya camera linapewa kipaumbele sana.
Muda huo hakukuwa na SUPER-AMOLED, display zinazotumika katika smartphones za hali ya juu(high-end) hasa Samsung wala IPS LCD zitumikazo hasa katika smartphones za Sony Xperia, HTC na nyinginezo. Displays nyingi zenye kuonyesha rangi(coloured displays) zilitumia teknolojia ya TFT(Thin Film Transistor) ambayo kwa siku hizi ni teknolojia inayokwepwa na watengeneza smartphones wengi, sababu kubwa ya kukwepa teknolojia hii ni kwamba hutumia nishati kubwa ya umeme na pia ina rangi hafifu katika muonekano wake(poor color saturation).
Nokia 6600 ilikuwa na internal memory yenye kiasi cha 6MB, na uwezo wa kuweka memory card hadi kiasi cha 32MB, kipindi hicho zikitumika memory card kubwa kwa umbo(macro sd card). Kwa muda huo internal memory hiyo ni kiasi kikubwa sana katika smartphone. Muziki au video hazikuwa zinahifadhiwa katika smartphones, ili kuweza kusikiliza muziki kwa ubora ilibidi kuwa na portable music player. Smartphone zilikuwa ni devices kwa ajili ya kazi za kiofisi sanasana.
Internet yenye spidi kwa kipindi hicho katika smartphones ilikuwa ni GPRS, na Nokia 6600 ilikuwa na GPRS(General Packet Radio Service) class 6 yenye uwezo wa spidi ya kudownload kati ya 24kbps hadi 36kbps(kilobyte per second). Tofauti kabisa na sasa ambapo flagship smartphones nyingi zinasupport huduma ya 4G LTE (Fourth Generation Long Term Evolution) ambazo spidi yake inafika hadi 50mbps(megabyte per second). Files nyingi zilizokuwa downloaded katika Nokia 6600 ni katika kiasi cha kilobytes tu. Ilikuwa ni shughuli kidogo pale unapotaka download file lenye 1.2mb(1229kb) kwa mfano, inaweza kukuchukua masaa na pengine na kusubiri kote huko file hilo lisiweze kukamilika.
Simu hii ilikuwa ikitumia operating system ya Symbian OS V7.0, Series 60 v2.0. Symbian OS haipo sokoni tangu mwaka 2013 ambapo simu ya mwisho kutumia operating system hii ilikuwa Nokia Pureview 808. Mtu yoyote ambaye ni mfatiliaji wa teknolojia ya smartphones anaweza kumbuka fika ni jinsi gani operating system hii ilivyokuwa ikipendwa na kutumiwa na watu wengi, ikumbukwe kwamba mnamo miaka ya 2004 hatukuwa na iPhones wala Androids, Symbian OS ndo alikuwa mtawala wa dunia katika smartphones. Kulingana na teknolojia ya kipindi hicho OS hii ilionekana kuweza kukidhi mahitaji ya watumiaji wa kila aina kwa kiasi cha kutosha.
Pamoja na kwamba miaka mingi imepita na teknolojia ya smartphones imekuwa bora maradufu. Lakini simu kama Nokia 6600 haitasaulika katika historia ya smartphones, sababu kubwa ni kutokana na misingi,mawazo na ubunifu iliyoleta katika uwanja wa kiteknolojia, muda huo Nokia ilikuwa ni kampuni ambayo inaona kesho na kuitendea kazi, ukilinganisha na makampuni mengi yalikuwepo muda huo katika upinzani kama BlackBerry na HTC(akitengeneza PDA[Personal Digital Assistant] za Windows Mobile), Nokia alikuwa muda wote hatua moja mbele, anaanza na wengi wanafata baada ya hapo. Mawazo ya Steve Jobs kutengeneza iPhone pengine yasingekuja kama Nokia asingetengeneza smartphone kama Nokia 6600. Pamoja na kwamba Nokia hayupo tena katika uwanja wa smartphones, lakini ubunifu na mawazo yake unaendelea kujidhihirisha siku hadi siku.
No comments :
Post a Comment