Dec 26, 2014

Mvumbuzi wa tovuti aongelea mustakabali wa mtandao kwa siku zijazo.

Tim Berners-Lee, ndiye mgunduzi wa kurasa za mtandaoni, zijulikanazo kama World Wide Website(www) au kwa kifupi Web. World Wide Website(www) ni moja ya nyenzo muhimu sana katika mtandao. Katika zama hizi za kidigitali ambapo kuna vifaa(devices) nyingi sana zinazotegemea matumizi ya mtandao, kunahitajika kuwepo na mabadiliko kila wakati ili kuendana na wakati.
Tim Berners-Lee


Suala la ukiukwaji wa sheria zinazosimamia internet privacy(faragha ya mtandao) ni moja la tatizo linalosumbua watumiaji wengi wa mtandao. Nchi kama Marekani wananchi wake huchunguzwa(Cyber Spying) na serikali yao kila wanachofanya katika devices zao zote zilizounganishwa katika mtandao bila ya wao kujua au kuombwa ruhusa, makampuni kama Apple, Google na mengineyo hushutumiwa kwa kutoa mwanya kwa serikali kuweza kufanya upekuzi huu wa taarifa za watumiaji wa mtandao
. Katika nchi zinazoendelea kama Tanzania, wengi wetu hatuchukulii maanani kabisa
utunzaji na kujua wapi panapotakiwa kushare taarifa zetu katika mtandao. Na ndo maana watu hushare namba zao za simu na taarifa mbalimbali katika mitandao ya kijamii bila shida, jambo hili si sahihi kabisa na linaweza kumgharimu mtu kwa kiasi kikubwa. Usalama mtandaoni ni moja ya vitu alivyozungumzia Berners-Lee.


Maswala mengine aliyoongelea mtaalamu huyu wa kompyuta kuhusu kesho ya tovuti ni kama haya:

  • Itahitajika kuwepo na muswada wa sheria ambazo zitawalinda watumiaji wa mtandao, waweze kujua pale taarifa zao zinapotakiwa kutumika na ni kwa ajili ipi na pia zitumike pale tu mtumiaji anapoidhinisha.
  • Taarifa kwa ajili ya umma zinatakiwa zipatikane kwa kila mtu bila kujali kipato au cheo alichonacho mtu huyo, katika nchi nyingi, taarifa zinazohusu umma zipo mikononi mwa watu wachache. 
  • Mabenki yanatakiwa kuboresha usalama. Benki nyingi huuliza taarifa nyingi za siri mfano password, si salama kushare taarifa kama hizo katika mtandao hata kama unazituma katika mamlaka husika.
  • Taarifa muhimu na za siri zinatakiwa kutunzwa kwa makini, mfano taarifa zinazohusu wagonjwa katika mahospitali. Zitumike kwa watu sahihi tu.
  • Devices zitumiazo mtandao kama vile kompyuta na smartphones zitazidi kuboreshwa muonekano wake kwa kukupa uhalisia zaidi na zaidi katika kutazama.  


No comments :

Post a Comment