Nov 20, 2014

Mambo si mazuri kwa Jeff Bezos safari hii.

Pengine ni mara yako ya kwanza kusikia jina hilo, lakini ushawahi sikia kampuni ya Amazon Online Retails. Bezos ndiye mmiliki na CEO wa kampuni hii maarufu sana duniani inayojihusisha na kunadi bidhaa mbalimbali kuanzia vifaa vya kielectroniki, vyakula vya viwandani na hadi mbolea kwa njia ya kuagiza mtandaoni. Kampuni hii imeanzishwa mwaka 1994 na tangu kuanzishwa kwake imekuwa ikipata mafanikio kadiri siku ziendavyo. Kilichomfanya Jeff Bezos kupata mafanikio katika kampuni yake ni kwa sababu ni mtu ambaye huja na mawazo tofauti na yenye kuleta hamasa sana. Amazon ni tofauti kidogo na online retailers wengine kwa mambo baadhi, ukiangalia gharama zao, huduma wanazotoa na mambo mengine mengi. Mpaka sasa, katika online retailers wote duniani, ni Amazon tu ndiye anatumia ndege ndogo zisizo na watu(Drones) katika kufikisha vifurushi kwa wateja wake, huduma hii inaitwa Amazon Prime.


Pamoja na kunadi bidhaa mbalimbali za makampuni mengine pia wana bidhaa zao za  kielectroniki ambazo huuza. Wanatengeneza tablets za Kindle Fire HD, HDX na ebook readers kama Kindle Paperwhite. Biashara ya hizi tablets na e-readers kiuhalisia imekuwa ikienda vizuri kabisa tangu kuanzishwa kwake. LAKINI, mwaka huu kuna jambo halijaenda sawa. Ni pale baada ya Amazon kuamua kujiingiza katika biashara ya kutengeneza smartphones. Uzinduzi huu umekuwa janga kubwa sana katika kampuni hii kibiashara.

Jeff Bezos akizindua Amazon Fire Phone.

Smartphone ya Amazon inayofahamika kwa jina la Fire Phone ilizinduliwa mnamo mwezi wa sita mwaka huu. Inapatikana rasmi nchini Marekani, Ujerumani na Uingereza. Baada ya kuingia sokoni kwenye mwezi wa saba hivi, ilileta tafrani kidogo kwa wale waliokuwa wakiingojea kwa hamu. Ni hali iliyozoeleka kwamba Amazon huuza bidhaa zake kwa bei nafuu na iliyo ya kuleta maana kwa hivyo watu walitegemea utaratibu utakuwa ni uleule katika mauzo ya Fire Phone, hali ikawa tofauti.

Kwa Marekani, Fire Phone ilikuja kupitia kampuni ya mtandao wa simu ya AT&T kwa kiasi cha dola za kimarekani $199(sawa na Tsh. 330,000) kwa mkataba wa miaka miwili.  Ni kiasi kikubwa au pengine sawa na mikataba ya flagship smartphones kama za Apple na Samsung, makampuni niliyotaja yamekuwepo kwa muda mrefu katika soko la smartphones na pia ni yenye sifa nzuri, ni ngumu kumfanya mnunuzi kutumia pesa nyingi kiasi hicho katika smartphone ambayo haifahamu kiundani halafu akaacha simu kama iPhone au Samsung Galaxy ambazo anazifahamu kwa miaka mingi. Watu wengi walitegemea Fire Phone itakuja katika gharama nafuu kabisa.

Pamoja na kwamba ughali wa simu hii ndiyo umepelekea mauzo hafifu ya bidhaa hii, lakini pia kuna sababu nyingine zilizochangia suala la mauzo hafifu.

Uhaba wa apps katika Amazon Appstore, Amazon ana online store ya applications ambazo baadhi hupatikana bure na nyingine zinakuhitaji kuzinunua ili uweze kuzitumia katika smartphone yako. Watumiaji wengi sana wa smartphones  hujali upatikanaji wa applications katika smartphone anayohitaji kununua. Appstore ya Amazon haivutii kwa sababu ina apps chache sana ukilinganisha na Google Play Store. Amazon ana takribani apps 240,000 katika store yake na wakati Google Play Store ina takribani apps milioni moja.

Firephone haisupport Google Play Services, katika smartphone hii huwezi kupata huduma za Google kama Google PlayStore, Gmail, Google Keep and Synchronisation ya data zako kupitia mtandao wa Google. Hii ina maana kwamba hutaweza kutumia apps zinazohitaji support ya Google Services kama Quizup, Google Play Music n.k. Ni adimu sana kwa flagship smartphone kukosa huduma muhimu kama hii, hasa ukiangalia smartphone wapinzani zote zina huduma hii.

Imechelewa sana kuingia sokoni, ukiangalia soko la sasa la smartphone limejawa na bidhaa nyingi mno kutoka makampuni mbalimbali. Samsung na Apple wakiwa wanaliongoza gurudumu hili. Nchi kama Marekani, Samsung na Apple wanachangia takribani asilimia 80 ya mauzo yote ya smartphones, asilimia inayobaki ikichukuliwa na makampuni mengine. Ni ngumu kwa Amazon kupata mpenyo wa kimasoko(business penetration) katika soko kama hili na pia ukizingatia bidhaa yao ipo katika gharama ya ghali.

Nadhani makampuni makubwa ya kiteknolojia yanahitaji kuwa makini katika kujaribu biashara mpya. Hii si mara ya kwanza kwa kampuni kama Amazon kufeli. Mnamo mwaka jana Facebook aliamua kutengeneza smartphone yake kupitia kampuni ya HTC, simu hii ilijulikana kama HTC First na kimsingi ilikuwa ni simu kwa ajili ya matumizi ya Facebook. Facebook alikuwa na mategemeo makubwa sana kutoka katika hii simu. Lakini haikuchuka muda mrefu mpaka simu kusahaulika kabisa katika ramani. Mifano hii inatuonyesha ya kwamba; katika biashara ya teknolojia, unaweza perform vizuri sana katika upande mmoja wa biashara lakini si kwamba ukijaribu upande wa pili, matokeo yatakuwa ni yaleyale. Jiulize, Samsung atapata mafanikio kama siku akiamua kutengeneza magari?. Usisite kutoa maoni au mchango wako hapo chini.


No comments :

Post a Comment