Nov 17, 2014

Jinsi ya kutuma files (pdf,doc,ppt,epub, n.k) kupitia WhatsApp Messenger.

WhatsApp ni moja kati ya instant messaging(IM) apps maarufu duniani na yenye watumiaji wengi sana, takribani watumiaji milioni 600 duniani kote. Ni IM bora ukilinganisha na zingine kwa kigezo kwamba ni rahisi katika kuitumia. Mbali ya kuwa na uwezo wa kukuwezesha kuwasiliana na watu mbalimbali, pia WhatsApp inakuwezesha kutuma na kupokea picha, video, muziki,namba za mawasiliano (contacts) na hata taarifa za mahali na uelekeo (location).

Pamoja na kukuwezesha kushare files za multimedia(music,photos, video), lakini kuna kasoro iliyopo katika app hii. Haina uwezo wa kutuma files zilizopo katika mfumo wa software(kama .exe, .apk, .bar n.k) na pia files katika mfumo wa
document(.docx, .pptx, .epub). Zipo njia baadhi zinazokuwezesha kutuma na kupokea mafaili ya mfumo huu, moja ya njia ambayo nadhani inafaa zaidi kutumia ni kwa kutumia programu ya kando (third party app) inayoitwa WhatsApp File Sender.

Kupitia WhatsApp File Sender unaweza kutuma mafaili kama hati za kiofisi(office documents) (.doc, .docx, pptx), pdf, .epub na kadhalika. Si hayo tu, kwa kifupi unaweza kutuma na kupokea kila aina ya faili kwa WhatsApp kupitia programu hii, NDIYO, KILA AINA YA FAILI. Unaweza kutuma hata programu kama .exe (executable), .zip na .apk au chochote kile unachotaka,

Namna Ya Kutuma Faili


1. Fungua WhatsApp File Sender, kisha      bonyeza "+" alama ya kuimgiza faili.
2. Tafuta faili unalotaka kutuma, kisha    "send"
3. Chagua "Share file with WhatsApp"
4. Chagua unaemtumia kisha "OK".

Kupokea Faili

1. Download faili kwa WhatsApp
2. Baada tu ya kudownload, WhatsApp File Sender
   itafunguka yenyewe na kuomba ruhusa yako ili
   kufungua faili hilo (decode). 

3. Elekeza sehemu unayotaka kuhifadhi hilo faili,        unaweza tengeneza folder lake maalum kwa ajli tu ya    kupokea mafaili kwa njia hii.
4. Kisha Ok.

  • WhatsApp File Sender hubadili mafaili (encoding) kwenda kwenda kwenye mfumo wa sauti (audio), na wakati wa kupokea hurudisha katika mfumo wake wa kawaida (decoding).
  • Kwa Kawaida WhatsApp hutuma faili lisilozidi ukubwa wa MB 16,lakini kwa njia unaweza kutuma faili lenye ukubwa wowote zaidi ya MB 16.
  • Unaweza tuma vitu vingi kwa mara moja, tengeneza folder la ".zip" weka mafaili yote ndani yake, kisha tuma.
  • WhatsApp File Sender hugawa mafaili makubwa katika ukubwa wa MB 16 kila moja, hii huwezesha kutuma mafaili makubwa zaidi. Mpokeaji ni lazima ahakikishe vipande vyote vimefanikiwa kuwa downloaded kabla ya decoding.
  • Njia nzuri kwa makundi ya WhatsApp kutumiana mafaili ya kiofisi kama notes na mengineyo kwa urahisi zaidi. 
    Download WhatsApp File Sender v1.5.2 HAPA


 Find it Useful/ Helpful? Fanya na wengine wafahamu pia. Share!! & Comment!!

No comments :

Post a Comment