Feb 20, 2014

Facebook anainunua Whatsapp hatimaye.

Mtandao wa kijamii wa Facebook umekubali kuinunua app maarufu ya kuchat ya Whatsapp. App hii itanunuliwa kwa kiasi cha dola za kimarekani $19 billion(trilioni 32 za Kitanzania), ni hela nyingi sana ukizingatia na kinachonunuliwa, kiasi hiki ni karibu na nusu ya thamani ya Kampuni ya BlackBerry. Mmiliki na CEO wa Whatsapp Bwana Jan Koum amesema bado wataendelea kufanya kazi kwa kujitegemea na pia hakutakuwa na matangazo katika kutumia Whatsapp. Facebook atatoa kiasi cha dola bilioni $4 kama fedha taslimu, $12 bilioni kama hisa na $3 bilioni kama hisa za Whatsapp ambazo atashikilia kwa miaka minne.



Ni swali la kujiuliza, kwa nini Facebook atatumia kiasi kikubwa sana katika ununuzi huu?. Katika kipindi kama cha miaka minne mtandao huu umekuwa katika ushindani mkubwa sana na mitandao mingi ya kijamii inayoibuka kila siku kutokana na kuwepo kwa teknolojia ya smartphone hasa za Android na Apple iOS, wachambuzi wengi wa teknolojia hutabiri kwamba kama Facebook hatobadilika  atapotea katika biashara. Vijana wengi wanahama Facebook sasa hivi na kuhamia mitandao kama Snapchat,Pinterest na mingineyo, na ili kujiweka sawa, ameamua kununua Whatsapp ambayo ina watumiaji wengi sana, takribani watumiaji milioni 450.

Ununuzi huu umekuja wiki moja baada ya Viber kununuliwa na Rakuten kwa kiasi cha $900 milioni, Viber ina watumiaji takribani milioni 300. Tofauti ya watumiaji milioni 150 lakini kwa kuuzwa wamepishana kiasi cha $18 bilioni, unaweza kuona ni jinsi gani Facebook alivyokuwa anakosa usingizi kwa sababu ya Whatsapp na akaamua kuinunua kwa gharama yoyote ile(overprice) . Una chochote cha kuongezea katika habari hii?, changia kwa kutoa maoni yako.

No comments :

Post a Comment