Feb 11, 2014

Billgates: Usiniite mtu niliyekimbia shule!

Umekielewa kichwa cha habari vizuri kabisa, William "Billgates" Gates ambaye anaongoza kwa utajiri duniani hapendi kuchukuliwa kama mtu aliyewahi kuacha shule. Mara nyingi huongelewa pamoja na watu kama marehemu Steve Jobs, aliyeanzisha Apple Inc. na Mark Zuckerberg ambaye ni mmiliki wa Facebook kama watu walioacha chuo na baadaye wakaja kupata mafanikio makubwa katika teknolojia.

Billgates

Billgates aliyasema hayo katika mahojiano ya Reddit AMA(Ask Me Anything) ambayo hufanyika kwa kuhoji watu maarufu na kuwauliza swali lolote lile. Alipoulizwa swali hili, "elimu ya chuo imekusaidia vipi katika kupata mafanikio uliyonayo sasa?", alijibu na kusema " ni ajabu kusema mimi niliacha chuo wakati nimesoma takribani miaka mitatu kiasi cha kuweza kuhitimu". Tajiri huyu ambaye ni mmiliki wa kampuni ya Microsoft amejizolea majina mengi sana akiitwa tajiri wa dunia, mtu mwenye uono wa mbali, mvumbuzi wa kipekee na hata msamaria mwema katika juhudi zake za kutoa misaada ya kibinadamu katika nchi nyingi masikini.

Kauli yake hii imekuja ikiwa ni siku chache tu zimepita baada ya Microsoft kumtangaza Mkurugenzi Mtendaji mpya Bwana. Satya Nadella aliyechukua nafasi ya Bwana Steve Ballmer. Billgates pia anaachia ngazi kama Mwenyekiti wa kampuni hii, si mtu anayefahamu sana kuhusu games pamoja ya kwamba kampuni yake inatengeneza game consoles za Xbox, alisema "Sijui sana kuhusu kucheza games, mwanangu wa kiume anafahamu mengi katika Xbox kuliko mimi".

Kuchaguliwa kwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Microsoft pengine kutaleta mabadiliko makubwa kwa kampuni hii. Nadella anaifahamu kampuni hii na amekuwa nayo kwa takribani miaka 22. Ukizingatia sasa Windows Phone OS inazidi kukua na pia wameinunua Nokia katika upande wa uzalishaji simu, na huku ndipo Nadella ameahidi kutilia mkazo sana. Mwishoni wa mwaka tutaweza kufahamu ufanisi wa bwana huyu.

No comments :

Post a Comment