Feb 7, 2014

Apple kutengeneza smartphone za Android,mmh!labda..........

Inashtua kidogo, lakini usishangae sana. Steve"Woz"Wozniak ambaye ni mmoja wa waanzilishi wa kampuni ya Apple sambamba na marehemu Steve Jobs ametoa maoni yake kwamba kampuni ya Apple wanaweza pia kutengeneza simu ambazo zitatumia Android OS na wakati huohuo wakiendelea kutengeneza iPhone. Ni ngumu kidogo kauli hii kuingia akilini aisee, na sidhani kama swala hili litakuja wezekana labda huko baadaye ambapo Apple maji yatamfika shingoni.
 Steve Wozniak kushoto akiwa na Steve Jobs kulia.

Anachodai Woz ni kwamba, Apple ni simu za tofauti na za aina yake, zina muonekano mzuri sana na mvuto wa hali ya juu, tofauti na mshindani wake ambaye ni Samsung, ukiwa na iPhone inayotumia Android itakuwa ni yenye utofauti mkubwa na Android zote zilizopo sasa. Pamoja na kwamba Woz ni mmoja wa waanzilishi wa kampuni hii lakini uhusiano wake wa sasa na kampuni hii ni kama walivyo wanahisa wengine tu Apple, kwa maana hiyo si kwamba kauli yoyote atayosema basi itafanyiwa kazi.

Mara kadhaa huwa anatoa kauli mbalimbali zinazoleta changamoto kwa Apple. Alishawahi kusema ya kwamba Windows Phone OS ina muonekano mzuri kuliko iOS, kudai kwamba iTunes inatakiwa pia kuwepo katika Android OS na kusema iPad zina ubora ambao haukidhi ushindani katika soko. Sidhani hata kidogo kama kampuni hii ya Cupertino itaweza kufikiria wazo hili, ila!siku za mbeleni unaweza ona kitu kama hiki kinatokea, Samsung ni mshindani mkubwa sana wa Apple, si Marekani tu bali dunia nzima. Mpaka sasa Samsung anashikilia 2/3 ya mauzo yote ya smartphone nchini Marekani, sasa kama hili hii itaendelea unadhani Apple atazidi kuwa kinara? itambidi atafute mbadala wa kujinasua, na hapo ndipo Android OS atapoonekana ni msaada pekee.

No comments :

Post a Comment