Mnamo mwaka 2007 ambapo marehemu Steve Jobs ambaye ni mmoja wa waanzilishi wa kampuni ya Apple Inc. alipozindua iPhone ya kwanza,Google nae muda huohuo alikuwa na mkakati wa kuzindua simu yake ya kwanza ya Android.
![]() |
Marehemu Steve Jobs akizindua iPhone ya kwanza kabisa |
Lakini baada ya Google kuiona iPhone,walisikia aibu kwelikweli kwa walichokuwa wamekiandaa ambacho ndo ingekuwa simu ya kwanza ya Android ambayo ingeshindana na iPhone.Ikabidi mpango mzima uanze tena upya na mfano(prototype) mwingine wa simu utengenezwe ili kuweza kuendana na ushindani katika soko.
Mmoja wa wahandisi wa Google waliokuwa wanasimamia mradi huo alisema"simu yetu ilikuwa mbaya sana ukilinganisha na iPhone tuliyoona Steve Jobs kashika,ilikuwa inafanana na BlackBerry hivi,bila touchscreen na iliyojaa vitufe vya kubonyezea(keypads)."
![]() |
Mfano(prototype) wa kwanza kabisa wa simu ya Android. |
Ndo maana ilichukua takribani mwaka mmoja baada ya iPhone kuzinduliwa na ndipo tukaona simu ya kwanza ya Android iliyokuwa ikijulikana kwa jina la HTC Dream au HTC G1(nchini Marekani kwa mtandao wa simu wa T-Mobile) ikitumia Android OS version ya Cupcake.Inaonesha wazi kabisa Google alikuwa na mpango wa kutoa simu yake akifata misingi ileile kama ya BlackBerry.Ikumbukwe enzi hizo BlackBerry alikuwa juu kabisa(heyday).Lakini iPhone ilibadili mawazo yao.
![]() |
HTC Dream,simu ya kwanza ya Android iliyozinduliwa mwaka 2008. |
Ni sahihi kusema kwamba Apple Inc. ndo wameleta mapinduzi makubwa sana katika teknolojia ya smartphones.Wamehamasisha makampuni mengi sana.
No comments :
Post a Comment