![]() |
Moja ya MP3 players za mwanzo kabisa,ikitengenezwa na kampuni ya Sony. |
Miaka minne baadaye,teknolojia ikapiga hatua. Mnamo mwaka 2001 Siemens SL45 ilizinduliwa ikiwa ni simu yenye uwezo wa kucheza muziki katika mfumo wa MP3. Lakini uzinduzi wa simu hii haukuweza fanya MP3 players kupoteza umaarufu wake na matumizi yake ya kila siku. Vikwazo vilivyokuwepo katika simu hii ni kwamba,ilikuwa na uwezo mdogo sana wa kuweza kubeba nyimbo(memory capacity) na pia ilikuwa na battery yenye uwezo mdogo wa kuweza kuhimili kupiga simu,kutuma ujumbe mfupi wa maneno na wakati huohuo kuweza kusikiliza muziki. Lakini pamoja na vikwazo hivi lakini huu ndiyo ulikuwa mwanzo wa teknolojia ya muziki katika simu.
![]() |
Siemens SL45,simu ya kwanza kabisa inayocheza muziki wa mfumo wa MP3. |
Miaka ikazidi kusonga mbele. Ikafika muda ambao simu kuweza kucheza muziki ikawa ni kitu kilichozoeleka,lakini bado watu waliendelea kutumia MP3 players zao kama kawaida. Sony Ericsson wakazindua simu aina ya W800i,simu hii ilikuwa ya tofauti kabisa na simu nyingine zilizokuwepo wakati huo zenye uwezo wa kucheza muziki. Iliweza kutunza miziki mingi,kukaa na chaji kwa muda mrefu huku ukipiga simu,kutuma SMS na kusikiliza muziki.
![]() |
Sony Ericsson W800i. |
iPod nazo zikazidi kuboreshwa tangu kuonekana kwa mara ya kwanza mwaka 2001,zilivuta makini ya watu wengi. Hali hii ilikuja badilika mnamo mwaka 2007 ambapo Apple alizindua simu ambayo ni smartphone inayoitwa iPhone.Sasa simu zikawa tena sio za kawaida bali ni erevu(smartphone). Aliyependa iPod ni wazi kuwa anapenda bidhaa za Apple kwa hiyo ataanza kutumia iPhone,kama atatumia iPhone hawezi kuona umuhimu tena wa iPod yake na wakati yote anaweza kuyapata katika simu moja. Tofauti na hapo ilipombidi kuwa na simu ya mawasiliano na kuwa pia na MP3 player.
Toka kuzinduliwa kwa iPhone mwaka 2007 na ndipo safari ya teknolojia ya smartphone ikaanza.Mwaka mmoja baadaye ikaja Android smartphone ya kwanza,HTC G1. Kila mtengeneza simu akaja na smartphone yenye uwezo mkubwa na wa kisasa wa kuweza kucheza muziki. Ikawa tena sio kuweka miziki kumi katika simu yako bali mamia ya miziki. Huku ukiwa na uwezo wa kusikiliza kwa muda mrefu sana bila chaji kuisha.
![]() |
iPhone ya kwanza,ikitumia mtandao wa 2G. |
Hivi leo kila mtu anasikiliza muziki katika smartphone na sio MP3 player tena. Hakuna anayehitaji tena MP3 player. Smartphones zinakuja na teknolojia ya hali ya juu ya muziki. Mambo yote yamekuwa rahisi,ni swala la kuingia tu katika mtandao na kudownload muziki wowote unaotaka na baada ya hapo kusikiliza katika simu yako.
Teknolojia ya smartphone imebadili muonekano wa vitu vingi ambavyo vilikuwa ni mazoea katika maisha ya kawaida. Huitaji tena kwenda cafe kwa ajili ya kuwekewa miziki katika MP3 player yako. Unapokuwa na smartphone kila kitu kipo katika simu yako,kupitia internet dunia nzima inakuwa katika kiganja chako.
No comments :
Post a Comment