Katika kipindi cha karibuni kumekuwa na ripoti mbalimbali zikiongelea jinsi gani idadi ya vijana wadogo hasa wale wa kati ya umri wa miaka 13-17 wanavyopungua katika namba ya watumiaji wa Facebook.
Ripoti ya hivi karibuni ambayo imetolewa siku ya Jumatano ya tarehe 15-Januari mwaka huu inaonesha mtandao wa Facebook ambao kwa sasa una takribani miaka kumi tangu kuanzishwa kwake ukipoteza namba kubwa sana ya vijana wanaoitumia. Ukiangalia takwimu zinaonesha watumiaji wa mtandao huu ukianzia Januari ya mwaka 2011 hadi Januari ya mwaka 2014 idadi ya vijana wenye umri wa miaka 13-17 imepungua kwa asilimia 25.3%,kwa vijana waliopo high school namba yao imeshuka kwa kiasi cha 58.9% na wale waliopo vyuoni ni kwa asilimia 59.1%.
Kutokana na takwimu hizi,mtandao huu ulijibu kwa kupitia msemaji wake na kusema ya kwamba" hatuna takwimu zetu kwa sasa zinazoonesha idadi ya watumiaji wetu kwa rika".Akaendelea zaidi kwa kusema"tunacholenga zaidi ni kuongeza na kuboresha huduma zetu kwa kuzingatia watumiaji wote,ikiwa pamoja na vijana wa chini ya miaka 20". Kauli hii inaonesha wazi kwamba wametambua swala hili la kupungua kwa watumiaji,lakini hawataki sema wazi bali kulishughulikia chinichini.
Pamoja na haya yote.Unajiuliza swali"ni kwanini hili linamtokea Facebook?",naweza fananisha kwa kiasi fulani yanayompata sasa ni kama yaliyompata BlackBerry mwaka 2007.Facebook ina miaka kumi sasa,tunaweza sema ni mtandao mkongwe,karibu nusu ya miaka aliyonayo Internet.Hivi karibuni kumekuwa na mitandao mingi sana mipya ya kijamii inayotoa huduma kama ya Facebook na pengine zaidi ya Facebook,mfano Snapchat,watumiaji wengi sana wa mtandao huu ni vijana kuanzia miaka 13 hadi 30 na kila siku watumiaji wanazidi kuwa wengi wengi.Unaweza kuona kwamba watumiaji wa Facebook wanakimbilia wapi.Pia kuna mitandao ya instant messaging kama Whatsapp,Viber,Hike na mingine mingi,unatuma sms na mtu anaipata muda huohuo tofauti ya Facebook kama ukituma sms kwa mtu asiye na smartphone au app ya Facebook Messenger basi ataiona mpaka atapotembelea mtandao huo.
Vijana wengi wanapenda kile kilicho kipya na cha kisasa zaidi.Kwa hiyo wanachofanya ni kuhama na kujaribu kilicho kipya.Pale anapoona kinafaa zaidi ya kile cha zamani,hapo ndipo cha zamani kinakosa soko. Mtandao wa Facebook una changamoto kubwa sana katika kuchuana na mitandao hii mipya ambayo imekuja ikizaliwa na mama ambaye anaitwa "Smartphone Technology".
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment