Jan 4, 2014

Alicia Keys anaondoka BlackBerry.

Alicia Keys katika uzinduzi wa smartphone za BB1O
Msanii,mtayarishaji wa muziki na mtunzi wa mashairi Alicia Keys anaondoka katika kampuni ya BlackBerry.Mwaka mmoja uliopita alikodiwa na kupewa nafasi kama Mkurugenzi wa Ubunifu Kimataifa katika kampuni hii akitangaza smartphone mpya za BlackBerry 10.Anafata katika orodha wa viongozi baadhi waliondoka katika kampuni hii akiwemo Thorsten Heins aliyekuwa CEO  wa kampuni hii.

Alicia Keys anaondoka BlackBerry huku akiwa na doa katika nafasi aliyokuwa akishikilia.Hapo mwanzo wakati anaanza kazi yake ya kuzitangaza smartphones za BlackBerry 10 aliwahi kutweet katika mtandao wa Twitter kwa kutumia iPhone na wakati alitakiwa kutumia BlackBerry Z10,smartphone ambayo alikuwa akiitangaza,swala hili lilizua mzozo sana.Alijitetea kwa kudai kwamba akaunti yake ilikuwa hacked. na si yeye aliyetweet.

Msemaji wa kampuni ya BlackBerry alisema kwamba"tumemaliza ubia wetu wa mwaka mmoja na Alicia Keys".Hakusema zaidi kwamba ni sababu gani iliyosababisha kuondoka kwa msanii huyu.Nadhani nyimbo yake haitakiwi kuitwa "Thi Girl Is On Fire" bali "This Girl Has Been Fired",usitilie maanani!ni utani tu!

No comments :

Post a Comment