Dec 23, 2013

Whatsapp messenger imefikia takribani watumiaji milioni 400.

App maarufu ya kijamii inayojulikana kwa jina la Whatsapp messenger imefikia kiasi cha zaidi ya watumiaji milioni 400.Kiasi hiki kimeongezeka watu milioni 50 zaidi ukilinganisha na kiwango kilichotajwa mwezi wa kumi mwaka huu na jarida la Forbes.

Kiwango hiki bado hakijafikia kiwango cha watumiaji wa mtandao wa Facebook ambao ni zaidi ya watu bilioni 1.2.Whatsapp imekuwa haraka katika kipindi kifupi sana cha muda.Hii inatokana na urahisi wake katika kuitumia ukilinganisha apps nyingine kama Viber,WeChat,Line n.k.

Pamoja na kutofikia kiwango cha watumiaji wa Facebook,lakini inazidi Facebook kwa kitu kimoja.Karibia sms bilioni 20 zinatumwa kwa siku na Whatsapp,hiki kiwango ni sawa na mara mbili ya kiwango cha Facebook kwa siku.

App hii inapatikana katika simu za BlackBerry,Nokia,Android na iPhone.Imezinduliwa mwaka 2009 na waliokuwa wafanyakazi wa Yahoo.Ina kazi kubwa katika kushindana na apps zingine za kuchat.Kila kukicha apps za mfumo kama huu zinaibuka,ushindani unaongezeka zaidi na zaidi.

Ni vizuri kunapokuwa na ushindani,hali hii inafanya kila mtengeneza app awe mbunifu zaidi na zaidi.Kila mmoja anataka kutoa kile kilicho bora kwa watumiaji.Kwa hali hii,unakuta kwamba watumiaji wanakuwa na machaguo mengi ambayo ni bora.Sasa,kuna app nyingi sana za kuchat ni swala la wewe mtumiaji kuchagua ile yenye urahisi kwako katika kutumia.

No comments :

Post a Comment