Dec 22, 2013

Mwaka 2013 unaishia,tutegemee nini mwakani katika teknolojia ya smartphone?

Mwaka 2013 ni mwaka ambao karibia makampuni yote ya kutengeneza smartphone yalikuwa bize.Mengine katika ubize wa kuhakikisha wanazidi kuwa juu kila siku na kuvuta watumiaji wengi,mfano Apple na Google(Android),wengine wakiwa bize kuhaha kampuni zao zisije kufa,mfano BlackBerry.

Tumeona hatua kubwa sana iliyopigwa katika teknolojia hii ya smartphone.Kila mtu kajitahidi kuonesha kwamba teknolojia inakua kwelikweli na pia yeye ndo mwenye uvumbuzi bora kuliko wenzake katika ushindani.
  • Apple kuleta smartphone ya iPhone 5S yenye processor ya 64bit.
  • Samsung na LG watengeneza simu ambazo kioo chake kimejikunja(curved display)
  • LG waleta teknolojia ya self-healing ambapo simu ya LG G Flex ikichubuka,ule mchubuko unapona ndani ya sekunde chache na panakuwa kama hapajachubuliwa.
  • Simu nyingi ambazo zinazuia maji kuingia ndani zimezinduliwa mwaka huu,mfano Samsung Galaxy S4 Active,Sony Xperia Z.
  • Camera za smartphone zina pixels kubwa sana kiasi kwamba mahitaji ya digital camera yanapungua,unahitaji simu tu kupiga yenye ubora kabisa.
  • Makampuni kama Sony,Samsung wameleta saa ambazo ni smart,zinatumika kama zilivyo smartphone ila yenyewe ni saa na unaivaa mkononi.Unaweza access chochote kilichopo katika simu yako kupitia saa hiyo.Samsung wanaziita Smartgear.
Hizo ni baadhi ya vumbuzi tulizoona mwaka huu.Lakini tunatakiwa jiuliza pia.Je!mwakani tutaona nini kipya cha kuvuta macho yetu?

Kampuni kama Apple na Android wenyewe hawana matatizo makubwa kama ilivyo kwa BlackBerry au Microsoft.Maana yake wana muda mwingi wa kuwaza mambo mazuri kabisa ya kuwaletea watumaiji wa bidhaa zao.

BlackBerry atatumia mwaka ujao kupona kutoka katika maumivu makubwa aliyopata mwaka huu,kwa hiyo kwa chochote atachofanya kitakuwa ni kama utangulizi.Atachofanya ni kupita katika njia zilezile alizopita Google mpaka leo na kupata mafanikio makubwa kiasi hiki katika Android,kwa hiyo sidhani kama atakuja na kitu kikubwa cha kutisha.

Windows kwa sasa anaonesha kukua kwa kasi kidogo,si mbaya.Kuna nchi huko Ulaya ambapo simu zake ni maarufu kuliko iPhone mfano baadhi ya sehemu nchini Italy.Nokia anazidi kutoa simu za Nokia Lumia ambazo zina ubora sana,tabs za Microsoft Surface na pia tabs za Nokia,ingawa bado ndo zinatafuta umaarufu.Labda mwakani atakuja na kitu kipya katika OS yake ya Windows Phone.

Kuna kampuni chipukizi nazo ambazo zinaonekana zikiwa na kasi nzuri,mfano Jolla wanaotengeneza simu za Jolla zinazotumia OS ya Sailfish,Mozilla Firefox nao wana OS yao inaitwa Firefox OS.

Kutakuwa na teknolojia nyingi sana za kusisimua mwakani,usishangae kuona simu ambayo ni kama kioo(transparent) lakini inafanya kazi zote za smartphone pamoja huoni battery wala sakiti.


No comments :

Post a Comment