Dec 1, 2013

Watengenezaji wa Sailfish OS wanataka install OS hii katika simu za Android.

Sailfish OS ni moja kati ya Operating Systems za Smartphone ambazo zimeanza hivi karibuni ikiwa pamoja na Tizen OS na Firefox OS.Ina kazi kubwa katika kushawishi soko ambalo asilimia 81% inachukuliwa na Android OS,asilimia 13% ikichukuliwa na Apple iOS na asilimia inayobaki BlackBerry,Windows Phone na hawa wengine kama Symbian OS wanakamilisha.

Mfumo wa OS hii unaruhusu mtumiaji ku-install apps za Android.Hii inampa uhuru wa kutosha mtumiaji wa simu hii katika kupata apps azipendazo.Hali hii inaweza kuvuta watu wengi ambao wamechoshwa na Android OS lakini kwa wakati huohuo bado wanataka endelea kutumia apps za Android.

Watengenezaji wa OS hii wanataka kwenda katika hatua nyingine zaidi.Wanachotaka kufanya ni kuiwezesha OS hii kuwa installed kwenye smartphones za Android.Kama swala hili litawezekana ina maana mtumiaji atakuwa OS mbili katika simu yake na ataweza tumia zote.

Si kazi kuinstall OS nyingine katika Android smartphones kwa sababu tayari kuna watengeneza software kama Cyanogen ambao hutengeneza OS za Android zisizo rasmi(Custom ROM) na huwa installed katika simu za Android baada ya simu hiyo kuwa rooted.

Sailfish OS nao wanaweza tumia mfumo huohuo kama wa Cyanogen au wa aina nyingine ambao utawezesha kuwa na OS mbili kwa wakati mmoja.Tatizo linaweza kuja kwa Google mwenyewe katika kuidhinisha kitu kama hichi.Google huwa ni muoga sana anapoona anaweza kupitwa na washindani wenzake katika biashara,miezi kadhaa iliyopita alimuwekea vikwazo vingi sana Microsoft katika Windows Phone.Hali hii ilikuja baada ya Microsoft kutengeneza app ya Youtube mwenyewe bila kibali cha Google ambao ndo wamiliki wa bidhaa hiyo.

Ni hatua sana katika ulimwengu wa kidigitali tulionao sasa.Mpaka sasa kuna OS za smartphones zipatazo nane na watengeneza smartphones zaidi ya 50.Hii inaashiria baada ya miaka michache tu kila mtu ataweza kumiliki smartphone.


No comments :

Post a Comment