Dec 4, 2013

Google wajikita katika teknolojia ya roboti,inasimamiwa na aliyevumbua Android.

Bwana Andy Rubin ambaye ndiye aliyesimamia mradi wa Android na mpaka leo umefika hapa anakuja na mradi mwingine wa kutengeneza roboti.Hapo nyuma aliondoka katika nafasi ya Android Chief na kumuachia Bwana Sundar Pichai ambaye anashikilia nafasi hiyo mpaka sasa,Bwana Sundar alikuwa akiongoza mradi wa Chrome kabla ya hapo.

 Kampuni ya Google ina miradi mingi sana.Na inaonekana mingi itakuwa ikianzishwa na Bwana Andy Rubin na kusimamiwa pia,hii inatokana na mafanikio makubwa aliyoleta katika mradi wa Android.

Bwana Rubin alishawahi kuwa engineer wa roboti katika kampuni ya Carl Zeiss(watengenezaji wakubwa duniani wa lens za kamera) kabla ya kujiunga na Google.

 Wanachotaka kukifanya Google ni kuongeza automation katika mifumo mbalimbali aitha ya kiwandani na hata majumbani.Kitu ambacho tunaona hata Amazon wanakifanya baada ya kutangaza kuanza kutumia Drones(ndege zinazoendeshwa na remote bila kuwa na dereva ndani yake) katika kusafirisha vifurushi.

No comments :

Post a Comment