Nov 29, 2013

Wafanyakazi wa zamani wa Nokia wazindua smartphone.

Siku kadhaa zilizopita,niliongelea jinsi kampuni za kiteknolojia zinavyochipuka nchini Finland.Wengi wa waanzilishi wakiwa ni wafanyakazi wa zamani wa Nokia.Hawa ni wengine baada ya kampuni chipukizi kama Rovio na Supercell.


Timu ya wafanyakazi wa zamani wa Nokia wamezindua simu mpya ya mfumo wa smartphone.Simu hii inaitwa Jolla Phone,ikitamkwa Yol-la.Inatumia operating system(OS) iitwayo Sailfish OS,uzuri wa OS hii inaweza kutumia apps za Android OS karibia zote.Mpaka sasa watengenezaji hawa wameingia mkataba na makampuni mengi ya mtandao wa simu nchini Finland katika kuuza bidhaa hii,kwa siku za mbele wataingia mkataba na makampuni mengi ya mtandao barani Ulaya.

Wachambuzi wengi wa maswala ya teknolojia wanasema kwamba,simu hii itakumbana na changamoto kubwa sana katika soko ambalo limetawaliwa na Android pamoja na iOS.

Mmoja wa wavumbuzi wa simu hii Bwana Marc Dillon aliliambia shirika la utangazaji la BBC kwamba"nia ya simu hii ni kuleta uhuru na wepesi wa kutumia,tofauti na simu kama iPhone! na pia kuleta uhuru na wepesi zaidi ya uliopo katika Android,watumiaji wanaweza kupata apps zaidi ya sehemu moja"

OS hii ndiyo iliyokuwa mwanzo ikiitwa MeeGo OS ambayo ilionekana kwa mara ya kwanza katika simu ya Nokia N9-00.Nokia aliamua kuachana nayo baada ya mawazo yake yote kuyaweka katika kutengeneza Windows Phone.

Sehemu kubwa ya code za OS hii ni huru(open source) hii inaamaanisha yoyote anaweza kuongeza kitu ili kuikuza na kuboresha OS hii.Android OS nayo ipo katika mfumo huuhuu.

Ni ngumu kidogo kusema kwamba OS itafanikiwa au la,kwa sasa ni mapema mno kutabiri.Lakini kwa mtazamo wangu.Nadhani Jolla itafanikiwa na hasa itachukua watumiaiji wengi wa simu za Windows Phone na BlackBerry.



No comments :

Post a Comment