Dec 17, 2013

Nokia atazindua simu ya Android iitwayo Normandy,ikiwa ni ya hali ya kawaida(low-end)

Nokia ana mpango wa kuzindua simu ya kawaida ambayo itatumia Android OS,itaitwa kwa jina la Normandy.Simu hii imeonekana katika mtandao wa evleaks kwa mara ya kwanza ikiwa na mfanano na Nokia Asha 501.Inaonekana kuwa ni ya kiwango cha kawaida kwa sababu haina flash ya kamera na mara nyingi smartphones zisizo na flash huwa ni za hali ya kawaida.

Simu hii itatumia Android OS lakini ambayo iko full customised,maana yake ni kwamba inaweza inafanya kazi zote za Android OS lakini ikatumia icon zilezile zinazotumika katika Nokia Asha smartphones au za aina nyingine ambazo si za kawaida katika Android.Kitu ambacho kinafanyika katika tablets za Amazon ziitwazo Kindle Fire.


Nokia anafanya hivi ili kujaribu kuona soko litapokea vipi smartphone ya brand yake huku ikitumia Android,tumezoea kuona smartphones za Nokia zikitumia Symbian OS na Windows Phone OS.Ndo maana kaogopa kuzindua simu ya hali ya juu akaishia pata hasara baada ya kukosa wateja.Kitu kilichomtokea  BlackBerry alipozindua BlackBerry Z10 na ikaishia kukosa wateja na kuingizia kampuni hasara ya mamilioni ya dola za kimarekani.Hii ni sababu inayofanya simu hiyo kuwa na vitu muhimu tu(basic low end smartphone features).

Kuna tetesi kwamba Nokia alikuwa na mpango wa kutumia Android katika simu zake za Lumia lakini alipiga chini mpango huo baada ya Microsoft kuleta dili ya Windows Phone OS.Hii haijasaidia lolote kampuni ya Nokia.Anahaha sasa na ndo maana anachukua maamuzi kama haya.Tuone kama simu hii itapokelewa kwa mtazamo hasi au chanya kwa watumiaji.

No comments :

Post a Comment