Dec 18, 2013

Je,watengeneza smartphone wanayajua mahitaji hasa ya watumiaji wa smartphone hizo?

Teknolojia ya siku hizi katika mapinduzi haya ya kidigitali tuliyonayo,si ajabu kuja kuona simu ambayo utaweza kuvingirisha kama bangili mkononi pale ambapo umemaliza kuitumia badala ya kuiweka mfukoni.

Tunaona makampuni kama Samsung,Sony na mengineyo wanakuja na bidhaa waziitazo Smartgear.Hizi ni saa za mkononi ambapo utaivaa na kuweza  kuaccess chochote kile kilichopo katika simu yako.Inaunganishwa na simu yako kwa kupitia nija ya Bluetooth au Wi-Fi.Ina display kama ile inayotumika katika smartphone.Pia,kuna teknolojia nyingine kama ya display iliyojikunja(curved display) ambayo ipo katika simu kama LG G Flex.

Swali linakuja,tunazihitaji sana hizi teknolojia na nyinginezo za mfumo huu?Kimsingi,hatuzitumii hata kama zikiwepo katika simu zetu.Sidhani kama ni teknolojia zenye manufaa katika kufanikisha kwamba mwisho wa siku tunakamilisha shughuli zetu zinazohusisha smartphones.

Watumiaji wengi wanataka betri yenye nguvu katika simu zao ambayo itakaa kwa siku badala ya masaa.Tatizo ni kwamba,teknolojia ya display imepiga hatua sana na hata ya processor lakini teknolojia ya betri ni ileile tangu miaka ya 2000.Wanachofanya ni kutengeneza betri kubwa ambayo nayo itakaa kwa siku moja na pia inaongeza umbo la simu,mfumo wa teknolojia ya betri unaotumika sasa uko hivi"kadiri betri inapokuwa kubwa na ndivyo uwezo wa kutunza chaji muda mrefu na unakuwa mkubwa"

Kinachohitajika kuonekana katika teknolojia ya simu ni mapinduzi ya hardware katika upande wa betri.Kama watengenezaji watakuja na mawazo mapya na yakafanikiwa katika kubadili ubora wa betri za smartphones,basi hii itakuwa ni furaha kwa kila mtu.Nina imani kubwa hichi ndicho kiu kikubwa cha watumiaji wote wa smartphones.

No comments :

Post a Comment