Dec 28, 2013

Kwa nini hii mitandao ya kijamii inajikita hasa katika mfumo wa sms?

Kuna ongezeko kubwa sana la mitandao ya kijamii sasa.Na mingi inayoanzishwa ni ya mfumo wa kutuma ujumbe mfupi(sms) mfano Wechat,Line na mengineyo.

Katika kipindi cha miezi miwili iliyopita,kumekuwa na mabadiliko makubwa sana katika nyanja hii.Mitandao kama Facebook,Instagram,Snapchat na Twitter imeongeza function ya kuweza kutuma sms kama ilivyo kwa mitandao mengine kama Whatsapp,Viber na kadhalika ambayo kwa sasa nayo iko bize kuhakikisha haipotezi watumiaji wake kutokana na ushindani mkubwa uliopo.


Siku mbili kabla ya Instagram Direct(feature ambayo inakuwezesha kuwasiliana na marafiki katika Instagram kwa kuwatumia picha na video) kuzinduliwa Twitter aliboresha feature ya kutuma sms katika app yake kwa Android na iOS.Facebook alibadili kabisa muonekano(User Interface) wa app yake iitwayo Facebook Messenger na kuongeza features nyinginyingi.Mwisho wa mwezi wa kumi Whatsapp Messenger ilitangaza kuwa na watumiaji wanaofikia milioni 400,milioni 150 zaidi ya watumiaji waTwitter.

Ni vigumu kutabiri ni app ipi hasa itayoweza kusonga kwa kipindi kirefu na kupata mafanikio zaidi na zaidi.Lakini inawezekana kwamba watu baadaye wakaja kuchoshwa na app ambazo zinawezesha kuchat kwa sms tu kama Whatsapp na kuhamia katika mitandao mingine kama Facebook na Twitter ambayo inatoa huduma zaidi ya moja.

Baadhi ya watu wanapenda faragha(privacy) na ndiyo maana wengine wanapendelea kutumia apps kama BBM.Lakini si wote wanaopendelea mfumo huu,watu wengi wanapenda kukutana na watu wengi na kwa  urahisi zaidi.Kwa hali hii mitandao kama Twitter,Instagram na Facebook pengine ndiyo itafanya vizuri mwaka 2014.

No comments :

Post a Comment