Dec 21, 2013

BlackBerry amesaini mkataba na kampuni ya Foxconn katika utengenezaji smartphones.

Naweza kusema kwamba mwaka 2013 ulikuwa ni mwaka wa mkosi kwa kampuni hii ya Canada.Tangu robo ya pili ya mwaka huu ilipoanza na ndipo mambo yao yote yakaanza kudorora,wamepata hasara ya mamilioni ya dola za kimarekani katika kipindi hiki cha takribani miezi nane.

Siku chache zilizopita waliingia mkataba na kampuni kubwa kuliko zote duniani ya kutengeneza vifaa vya kielectroniki ambayo makazi yake hasa ni Taiwan,Foxconn.Kampuni hii inafanyia sana uzalishaji wake nchini China,ina sifa nzuri sana kwa kutengeneza bidhaa bora za kielectroniki.Kiwanda hiki hakitengenezi bidhaa kwa nembo yake bali hupewa oda na kampuni nyingine katika kutengeneza bidhaa.Hapa ndipo iPhone na iPad zinapotengenezwa,game consoles za Xbox,kompyuta za HP na bidhaa nyingine nyingi.

Kimsingi,BlackBerry wameamua kufanya uamuzi huu ili kupunguza gharama za utengenezaji wa simu zao.Ukiangalia uzalishaji wao mkubwa huwa unafanyika nchini Canada,Mexico,Brazil na Hungary.Hizo nchi zote gharama za uzalishaji ziko juu ukilinganisha na kwenda kuzalisha bidhaa hiyohiyo ya smartphone nchini China.

Wanachokisema BlackBerry ni kwamba wanataka boresha zaidi bidhaa zao na pia kuongeza machaguo mengi kwa watumiaji,ina maana kwamba kutakuwa na aina nyinginyingi ambazo bei zake zitakuwa nafuu lakini ubora ukibaki palepale.Ukiangalia kwa sasa,simu zote za BlackBerry zinazotumia Operating System ya BlackBerry 10.2 OS ni za bei ya juu,bado hamna simu ambayo ni ya gharama nafuu.

No comments :

Post a Comment