Nov 6, 2013

Windows Phone zinaanza kupata kasi,ni maarufu kuliko iPhone nchini Italy.

Windows Phone zimeanza badili taswira yake katika kupendwa na watu wengi.Kwa sasa,nchini Italy ni maarufu sana kuliko iPhone.Na pia inaanza pata umaarufu mkubwa katika nchi nyingine nyingi za Ulaya.



Kati ya watu kumi wenye smartphones mmoja ni mtumiaji wa Windows Phone.Hii maana kwamba Windows Phone  inachukua asilimia kumi ya mauzo ya simu Ulaya.

Lakini pia simu hizi zinafanya vizuri sehemu nyingine mbali na Ulaya zenye masoko yanayochipukia kama Latin Amerika.Pamoja na Windows kufanya vizuri bado ipo nyuma sana ya Android ambayo mpaka sasa ina maana asilimia 71.9% katika bara la Ulaya.

Nchini China Android ina asilimia 81.1%.Hii inachangiwa sana na makampuni mengi ya China yanayotengeneza simu zenye ubora sana na zinauzwa humohumo nchini.Makampuni kama Xiaomi,Meizu,Lenovo na ZTE yamesaidia sana kuipa umaarufu Android nchini China.

No comments :

Post a Comment