Nov 1, 2013

Android 4.4 imetoka rasmi,ikipanga kufikia watu zaidi ya bilioni moja.

Kuzinduliwa kwa simu ya Google ya Nexus 5 kumeleta pia na uzinduzi wa Android version mpya ya Android 4.4 au kwa jina lingine Kit Kat.Jina la Kit Kat limetoka kwenye chocolate ya Nestle na nadhani Google wameona ni vyema kutumia jina hili kwa umaarufu zaidi wa version hii ya OS.

Google wamesema kwamba version hii itasupport simu nyingi hadi zile zenye RAM ya kiasi cha 512MB ambazo nyingi zao ni low end smartphones.
 Operating system hii imeboreshwa katika muonekano wake wake ikiwa na muonekano mpya kabisa katika app ya Phone.Utaweza kutafuta majina ya phonebook katika akaunti nyingine za Google hapohapo,kutafuta sehemu za karibu kwa kutumia GPS.

Kuna muonekano mpya pia wa app ya Google Hangout na sasa MMS na SMS zipo katika sehemu moja.Lockscreen iko na shortcut ya camera.
 Kuna feature nyingine mpya inayoitwa Airprint ambayo utaweza kuprint nakala toka katika simu yako kwenda kwenye printer bila kutumia waya(wireless printing),kwa sasa HP printers tu ndiyo zinakubali hii kitu.

 Kitu kizuri ni kwamba Version itafikia watu wengi sana,hadi wale wenye low end smartphones ila pamoja na kwamba Samsung Google Nexus ina RAM ya 1GB lakini haitapata update hii.





No comments :

Post a Comment