Nov 6, 2013

Mpango wa kununua kampuni ya BlackBerry umefeli,Heins nae afukuzwa.

BlackBerry ambayo zamani ilikuwa ikijulikana kama RIM BlackBerry ilitangaza hivi karibuni kuwa mmoja wa wamiliki wake wakubwa wa hisa anaweza nunua kampuni hii.Badala ya kuchukua hatua hii sasa wameamua kwamba kampuni ya Fairfax Financial itawekeza kiasi cha dola bilioni moja ili kuirudisha  kampuni kwenye mstari.

 Wakati hilo likifanyika,aliyekuwa CEO wa kampuni hiyo Bwana. Thorstein Heins ametuliwa kazi pamoja na Mwenyekiti wa bodi ya kampuni hiyo Bibi. Barbara Stymiest.

Ataechukua nafasi hiyo ni Bwana. John Chen,ambaye alishawahi kuwa CEO wa Siemens AG na Sybase,ni mtu wa muda mrefu sana katika teknolojia akiwa ni Profesa wa mambo ya umeme.

Kampuni ya Fairfax ilipanga kuinunua BlackBerry kwa kiasi cha dola za kimarekani bilion 4.7.Heins atapata kiasi cha dola za kimarekani milioni 22 kwa kuondolewa kwake.Hii itamfanya kuwa na kiasi cha pesa kinachofikia dola za kimarekani 56.

No comments :

Post a Comment