Nov 10, 2013

Kampuni ya BlackBerry inawezaje kujinasua toka kwenye majanga?

BlackBerry ambayo zamani ilikuwa ikijulikana kama RIM BlackBerry imepata jeraha baada ya jeraha katika hiki cha nyuma.Hii ikiwa ni kushindwa kuleta Operating System ya BlackBerry 10 kwenye tab zao za BlackBerry Playbook,kuchelewa ufikishaji wa app ya BBM katika Android na iOS na T-Mobile kuondoa baadhi ya simu za BlackBerry kwenye store zake za mauzo.
Katika kipindi cha miezi sita baada ya BlackBerry Z10 kuzinduliwa,kampuni ilianza poromoka kwelikweli.Ikipoteza karibia mabilioni ya dola za kimarekani.

Unaweza jiuliza,ni nini hasa tatizo la simu hii na Operating system mpya?Je!tatizo ni user interface ndo kilichoboa watu wengi?


 Hamna mtu anayetaka kusikia habari ya BlackBerry Z10 wala BlackBerry Q10.Ukiangalia simu kama Z10 ilikuwa ni flagship ya kampuni lakini ni tofauti kabisa ukiangalia na flagship za kampuni nyingine kama HTC One,Sony Xperia Z au Samsung Galaxy S4 katika hardware na software.Kwa hali hii ikashindwa kuchuana katika soko.

 Mpango wa kuliuza kampuni umeishia katikati na Mkurugenzi Mtendaji Bwana. Thorstein Heins akiondolewa na nafasi hiyo ikichukuliwa na Mkurugenzi mtendaji wa muda Bwana. John Chen.

 Kuna tetesi kwamba kampuni ya kichina ya Lenovo ina mpango wa kununua baadhi ya hisa katika kampuni hii.Inawezekana huyu ndiye akawa mkombozi wa kampuni hii.Iko wazi kabisa kama Lenovo ataweza nunua hisa na kupewa mamlaka katika kampuni hii basi muonekano wa simu za BlackBerry utabadilika maradufu.










No comments :

Post a Comment