Nov 18, 2013

Matumizi mbadala ya teknolojia yanavyobadili dunia kila siku.

Tabaka kati ya wagunduzi wa vifaa vya kiteknolojia na watumiaji wa vifaa hivyo linazidi kuongezeka kila siku.Inafikia mahala ambapo kifaa kinakuwa na matumizi mengi sana kuliko hata yale mgunduzi aliyafikiria wakati wa kutengeneza kifaa hicho.Haya ni baadhi ya matumizi mbadala.


 1.Smartphones zinatumika kama kikusanya taarifa za hali ya  hewa ,simu uliyonayo ndani yake imesheheni sensors nyingi sana ikiwamo zinazoweza kupima mwanga,joto,presha,nguvu ya usumaku na hata uelekeo.Taarifa zinazokusanywa na sensors hizi zinaweza tumika katika vituo vya utabiri wa hali ya hewa.Kampuni moja ya nchini Uingereza inayoitwa OpenSignal imetengeneza app inayoitwa WeatherSignal inayokusanya taarifa kutoka katika Android smartphones ili kuboresha utabiri wa hali ya hewa,swala hili limeonesha kuleta mafanikio sana katika ukusanyaji wa taarifa za utabiri wa hali ya hewa.

2.Matumizi ya Wi-Fi katika kuonyesha mahali ulipo(Location),mtandao wa Wireless Internet umewekwa mahususi kwa ajili ya mawasiliano ya internet bila kutumia wire wowote katika kupata mawasiliano,unatumika sana kwa sasa na kampuni kama Google na Navizon katika miji iliyoendelea yenye mawasiliano ya Wi-Fi katika sehemu kubwa kukuonyesha taarifa za mahali ulipo(Location).Teknolojia ya GPS kwa sasa imefanikiwa sana na hii pia imetokana na upatikanaji rahisi wa Wi-Fi katika sehemu nyingi.

3.Matumizi ya Twitter katika majanga, pamoja na kwamba ni mtandao wa kijamii na wengi hutumia sana kushare picha na kutuma ujumbe mfupi(kwa lugha maarufu watu husema "kutweet"),app hii pia huwa inasaidia sana katika majanga,ila hili halikuwa lengo kuu la mtandao huu.Husambaza taarifa kwa muda mfupi sana katika machafuko ya kisiasa,majanga ya asili na mambo mengine.Hata makundi ya kigaidi kama Al-Shabaab hutumia mtandao kutoa taarifa kwa dunia.

4.Kifaa cha Mosquito kutumika kutoa mlio wa kubugudhi, ni vigumu kuwazidi akili watoto wa kizazi hiki ambao wengi wanazaliwa na kukua na teknolojia,tofauti kwa watu wazima ambao teknolojia ya sasa inawapa shida sana kuendana nayo  na kwa wakati.Mfano mzuri ni kifaa kinachoitwa Mosquito ambacho hutoa sauti  inayosikika na vijana tu hasa wale chini ya miaka 18,sauti hii husumbua masikio ya anayeisikia na lengo lake ni kuzuia vijana kuzurura ovyo mitaani,lakini kampeni moja ilipinga kutengenezwa kwa kifaa hiki na kudai ya kwamba kinakiuka haki za binadamu,pamoja hakitumiki katika sehemu za wazi na mitaani bali hutumika mashuleni ambapo kwa wanafunzi wanaozurura ovyo huwasumbua masikio na hurudi kutulia darasani,ajabu ni kwamba walimu hawasikii kabisa sauti hii.

 5.iPad kwa ajili ya upasuaji wa mwili wa binadamu, madaktari wa upasuaji huko Ujerumani walipiga picha ya ini la mgonjwa wa kansa ya ini kwa kutumia iPad na kutumia picha hiyo kuona sehemu ambazo zimeathirika na kansa na pia kuona mishipa ya damu,picha hii iliyokuwa ya 3D iliwasaidia kuepuka kujeruhi ini wakati wa upasuaji.


Hayo ni baadhi ya matumizi mbadala ya teknolojia,tunaona ni kiasi gani teknolojia ilivyo pana.Kwa upande mwingine ni faida kubwa sana kwa baadhi ya watu na kwa upande mwingine ni hasara kwa watu wengine lakini cha msingi ni kwamba inazidi kurahisisha sana maisha.


No comments :

Post a Comment