Nov 11, 2013

Ahadi za Stephen Elon iwapo atachaguliwa kuwa CEO mpya Microsoft.

Miezi michache iliyopita CEO wa sasa wa Microsoft Bwana. Steve Ballmer alitangaza mwisho wa mwaka huu atastaafu kazi hiyo.Kauli hii ikaleta maswali mengi mojawapo likiwa,nani atakuwa mrithi wa huyu bwana?

 Siku chache zilizopita imetoka listi ya majina ya watu ambao huenda mmoja wao akachukua nafasi ya Ballmer.Listi hii imemtaja pia aliyekuwa CEO wa Nokia Bwana. Stephen Elop,Ballmer na Elop ni watu wa karibu katika kazi maana wao ndiyo walioshughulika na mpango mzima wa kuzaliwa kwa Windows Phone.
 Stephen Elop
Ahadi ambazo Elop amezitaja ni kuiuza Xbox na Bing,hiki ni kitu ambacho kwa muda mrefu sana wawekezaji kwenye kampuni ya Microsoft wanakipigania kifanyike.Bidhaa hizi mbili zinaonekana kuongeza mzigo mkubwa sana kwa kampuni.Baadhi ya watafiti wa uchumi wanasema ya kwamba,kwa kufanya hivyo Microsoft itaweza kuongeza mapato yake kwa asilimia 40%.Kingine ambacho Elop amesema ni kuboresha app ya Microsoft Office katika  Android na iOS ambapo kwa sasa app hii ina vitu vichache sana ambavyo ni msingi tu.Hii itaongeza umaarufu wa bidhaa za Microsoft kwenye Operating System nyingine kama Google anavyofanya kwa kuboresha zaidi app kama Youtube na Google Maps ambazo zipo kwenye Android na iOS pia.

 Mpaka sasa watu wengi wanampa nafasi kubwa Elop katika kuchukua kiti cha Ballmer,tusubiri kutoka kwenye uongozi wenyewe wa Microsoft wana uamuzi gani.CEO atatangazwa kabla ya mwaka huu kuisha.



No comments :

Post a Comment