Nov 12, 2013

BlackBerry OS 10.2 haitakuwa na Play Store,lakini itawezekana ku-install apps za Android.

Habari zimevuma kwamba OS version ya BlackBerry 10 itakuwa na Play Store app,lakini wenye kampuni wenyewe wamekanusha swala hili.


Sawa hakutakuwa na Google Play Store,bali itawezekana kuinstall apps za Android katika BlackBerry kwa kudownload file la Android app la extension ya .APK na kutumia file manager yoyote iliyopo katika simu ya BlackBerry kuinstall,njia ileile inayotumika katika kuinstall apps katika Android OS unapokuwa umedownload mbali na store za zilizopo.Njia hii inafahamika kama sideloading.

 Kitachowezesha kufanyika kwa hizi installation za apps za Android kwenye BlackBerry ni kuwepo kwa Android Runtime,hii itaruhusu app hizi kufanya kazi japokuwa sio katika OS mahususi.Kwa hiyo haitahitaji kuzibadili app hizo katika mfumo wa BlackBerry ambapo unatumia extension ya .BAR.

Hakutakuwa na widget za hizo apps kwa sasa,lakini kadiri siku zinavyoenda nadhani kitu hiki kitakujumuishwa.Ni hatua nzuri BlackBerry wanayofikia kwa sasa,wanaamua kulegeza kamba taratibu kuendana na matakwa ya watu wengi kwa hivi sasa.







No comments :

Post a Comment