Nov 12, 2013

"Hakuna Google Play Store kwenye BlackBerry OS 10.2",BlackBerry wasema.

Kauli hii imesemwa na mmoja wa wakilishi wa kampuni ya BlackBerry baada ya picha inayodaiwa kuonesha BlackBerry Z10 ikitumia Google Play Store kuonekana katika forum ya CrackBerry,lakini kitu hiki kimekanushwa na BlackBerry wenyewe.

 Watumiaji wa simu za BlackBerry zinazotumia BlackBerry OS 10 kwa sasa wanangoja update ya OS hiyo itayokuwa na jina la BlackBerry OS 10.2 na pengine ikawa inadhaniwa kwamba Play Store itakuwa ni moja ya apps katika update hiyo.
Nadhani BlackBerry anatakiwa kuchukua tukio hili kama moja ya wazo la yeye kuanza kutumia kutumia apps za Android na kuongeza uwanja wake wa kuwa na app nyingi zaidi,kwa upande wa pili BlackBerry imezidi kusema kwamba BlackBerry World itabaki kuwa ndiyo sehemu ya msingi na maalumu kwa watumiaji wa BlackBerry kudownload apps.


Labda pengine kwa siku za mbeleni kitu hiki kinaweza kufanyiwa kazi au BlackBerry akaja na mpango mwingine bomba zaidi katika kuvutia watu wengi kutumia bidhaa zake.

No comments :

Post a Comment