Oct 28, 2013

Ajabu!Lumia 800 yapiga kazi kama kawaida baada ya kupotea kwa miezi mitatu na nusu kwenye maji.

Inashangaza sana hii kitu,simu ya Nokia Lumia 800 imekutwa ikifanya kazi baada ya kuzama kwenye ziwa kwa miezi mitatu na nusu.

 Inaweza kuwa ngumu kuamini jambo hili.Imetokea huko Sweden na kisa hiki kimesimuliwa na Roger Nilsson katika ukurasa wake wa Facebook.Baada ya simu kudumbukia ziwani,ilijificha katikati ya miamba miwili.Baada ya kuokotwa ilikuwa imezungukwa magamba na Algae.Huyu bwana aliisafisha na baada ya kumaliza aliiweka kwenye chaji na simu ikaanza kuingiza chaji.



 Anadai kwamba mpaka sasa hamna tatizo lolote katika simu hiyo na inakaa na chaji siku mbili kama kawaida yake.

 Kama anachosema ni kweli,basi ni kitu safi sana kwa simu isiyokuwa na specifications za kuzuia maji kuweza kuhimili muda wote huo.Pia,itawapa sifa zaidi kampuni ya Nokia.

Kampuni nyingi kwa sasa wataanza tengeneza simu zao zikiwa na sifa ya kuzuia maji.Lakini itakuwa ni zile za hali ya juu(high end).



No comments :

Post a Comment