Oct 20, 2013

Smartphone tatu bora za kiwango cha kati(midrange) kwa sasa.

Inapofikia katika swala la kuchagua simu ipi ni bora kuna vitu vingi vya kuzingatia.Wengi huchagua simu kulingana na thamani ya pesa mtu aliyonayo.Mbali na hapo kuna vitu mtu ambavyo huangalia katika uchaguzi wa simu.

Simu nyingi ambazo ni za kiwango cha kati huwa na vitu vingi vinavyorandana,mara nyingi na sifa zinazofanana mfano kama kuwa kioo chenye ukubwa inchi 4.0 mpaka 4.3,pixel density per inch huwa ni kati ya 217 hadi 350,nyingi huwa na processor yenye CPU mbili(dual core processor),kama ni android basi huwa na version ya android 4.0(ice cream sandwich) au android 4.2(jelly bean),battery huwa na kiwango cha kati 1650mAh hadi 2000mAh.Kuna baadhi ya simu za kiwango cha kati zinakuwa na baadhi ya features za simu za gharama ya juu na pia nyingine za kiwango cha kati ila zinakuwa na baadhi ya features zaa kiwango chini(low end).

Kwa hivyo,uchaguzi wa simu unahitaji umakini kidogo ili kupata kitu kinachoendana na thamani ya hela yako pia upate simu itayoridhisha mahitaji yako.Hizi ni baadhi ya simu bora tano ambazo ni za kiwango cha kati ila ziko poa kwa kulinganisha gharama yake na yaliyomo katika simu.

1.Sony Xperia V-Uzuri wa simu hii ni kwamba haiingizi uchafu wala maji,ni mbadala wa Xperia Z.Inatumia operating system ya Android,ina kioo cha inchi 4.3(720X1280,342ppi,processor yake ni dual core ya Qualcomm Snapdragon S4 plus yenye speed ya 1.5Ghz kwa CPU moja.RAM yake ni 1GB na pia ina support mtandao wa 4G,Long Term Evolution(LTE).
2.Huawei Ascend P6-Katika hii simu Huawei kathibitisha wazi kwamba yupo fit katika kutengeneza smartphones.Mpaka sasa,ndio simu pekee nyembamba kuliko zote ikiwa na unene wa 6.18mm tu.
Ina processor yenye CPU nne(quad core processor) yenye spped ya 1.5Ghz ikiwa na RAM yenye 2GB,kioo chake kina ukubwa wa inchi 4.7 na ikiwa na 312ppi,imetumia teknolojia ya hali ya juu ya kutengeneza display yake,IPS+LCD capacitive touchscreen na pia inatumia Android 4.2.2(Jelly Bean)
3.Samsung Galaxy S4 Mini-Huyu ni mdogo wake kabisa na Samsung Galaxy S4,ina kioo cha ukubwa wa inchi 4.3 na pia 256ppi,imetumia kioo cha hali ya juu sana cha Super AMOLED,kioo hiki kina rangi nyingi sana tofauti na vioo vingine kama vya TFT au LED backlit na pia kinatumia nishati kidogo.Ina processor ya Quad core yenye speed ya 1.7Ghz.


No comments :

Post a Comment