Oct 19, 2013

Hizi ni Apps tano za Android hutakiwi kukosa kuwa nazo katika simu yako weekend hii.

Google Play Store ina apps nyingi sana ambazo ni nzuri na zinapatikana kwa bure na nyingine mpaka ulipie,kwa hii weekend hizi ni apps tano zitazofanya weekend yako kuwa poa kabisa katika kujiburudisha na smartphone yako ya Android.

1.Google Play Music-hii ni app ambayo baadhi ya simu nyingi huja nayo pale mtu anapoinunua(pre-installed app),ni kwa ajili ya kusikiliza muziki ulionao kwenye simu au pia kwenye mtandao.Ni rahisi kutumia na ina muonekano mzuri sana,muziki wake ni wa hali ya juu.Inapatikana bure kwenye Google Play.

2.Instagram-Hii ni maarufu sana na inafahamika na watu wengi,lengo lake kuu ni kushare picha pamoja na video fupifupi kati ya watumiaji.Hivi karibuni imeboreshwa baadhi ya vitu kama settings za video na jinsi kucontrol matumizi yako ya data na pia sasa unaweza straighten picha ambayo umepiga kwa kutumia app hii.Inapatikana bure pia.

3.Whatsapp-Hii pia ni maarufu,kwa ajili ya kuchat na ndugu,jamaa na marafiki.Imeboreshwa katika vitu vingi kwa kuwa na speed katika kurespond na mengineyo kama muonekano wake katika baadhi ya simu zinazorun Android 4.0 na kuendelea.Inapatikana bure kwa mwaka mmoja Google Play.

4.TED-Ni app ambayo unaweza download na kuangalia mtandaoni video mbalimbali zinazihusiana na mikutano ya TED,video hizi zipo katika makundi mengimengi,zina mafundisho na hamasa sana katika kujua mambo mengi duniani na jinsi kautafuta ufumbuzi wake,inapatikana bure.

5.Gmail-kutokana maboresho makubwa sana yaliyofanyika kwenye hii app kwa sasa ni rahisi sana kutuma na kupokea barua pepe za Google,kwa sasa unaweza tambua nani yapo online.App hii huja na simu(pre-installed)

No comments :

Post a Comment