Oct 20, 2013

Amazon washaanza kusafirisha tablet mpya za Kindle Fire HDX kwa wateja walioagiza mapema.

Kampuni ya Amazon imeanza safirisha tablet zake mpya lakini kwa sasa wataanza na tablet za inchi 7 kwanza.Hii ni kwa wateja wale walioagiza mapema tablet hizi.
Amazon walitangaza mnamo ijumaa wakisema kwamba wateja ambao walishaagiza tablet hizi mapema,zitawafikia hivi karibuni.Kwa wale wanaopanga kununua tablet hizo kwa sasa itawabidi wasubiri,uagizaji mwingine utaanza wiki ijayo.

Tablet hizi zitakuwa na sifa nyingi nzuri na huenda pia ndo zikawa tablet bora za Android kwa muda huu zikiizidi vitu vingi tu tablet ya Nexus 7 kizazi cha pili.Zenye inchi 7 zitakuwa na processor ya Quad core yenye speed ya 2.2Ghz kwa core moja na itatumia operating system ya Fire OS ambayo iko based na Android Jelly Bean 4.1.Inagharimu dola za Kimarekani $229 ambazo ni sawa ni SH.384,000/= za Kitanzania.

Wale wateja walioagiza tab hizi ambazo ni za inchi 8.9 itawabidi waendelee kusubiri mpaka Novemba 7 ambapo uagizwaji rasmi utaanza.

Kampuni ya Amazon kwa sasa imejikita sana katika kutengeneza tab za Android tofauti na hapo mwanzo ambapo walikuwa wakitengeneza tab kwa ajili ya kusoma vitabu na hata zisizo na rangi(black n white) na pia kuna uvumi wako katika mpango wa kutengeneza smartphones zao wenyewe.
 

No comments :

Post a Comment