Oct 18, 2013

Picha rasmi ya Nexus 5 yaonekana Google Play.

Katika wiki chache zilizopita mitandao mingi imekuwa ikionesha picha ya simu mpya ya Google ambayo itaitwa Nexus 5.Simu hii bado haijazinduliwa rasmi ila muonekano wake unafanana kama wa Nexus 7 kizazi cha pili iliyozinduliwa mwaka huu mwezi Juni.

Mtengenezaji bado ni yuleyule,LG.Simu hii imeonekana katika picha kwenye Play Store ikiwa pamoja na tablet za Nexus 7(kizazi cha pili) na Nexus 10.Ikioneshwa bei yake ya kununua ikianzia $349 ambazo ni sawa na 584,600 za Kitanzania.
Ni wazi bila shaka simu hii itakuja na version mpya ya operating system ya Android itayoitwa Android 4.4 au Kit Kat.

Muda wowote kuanzia sasa simu hii inaweza zinduliwa rasmi na Google.

No comments :

Post a Comment