Oct 3, 2013

Namba ya watoto wanaomiliki simu imeshuka.

     Kiasi cha watoto wanaomiliki simu za mkononi kimeshuka,na hii ikiwa ni mara ya kwanza kihistoria.
 Takwimu hizi zinatoka katika kampuni moja inayojihusisha na mambo ya takwimu iitwayo Ofcon.
 
     Asilimia 43 ya watoto wadogo wenye miaka kiuanzia mitano mpaka kumi na tano ndio sasa wanaomiliki simu,ukilinganisha na asilimia 49 ya mwaka jana.

Je!hii ina maana watoto wamepata michezo mingine inayowafanya waachane na simu?
Jibu ni Hapana!badala ya wao kutumia simu za mkononi kwa sasa,

mbadala umekuwa tablet computers. Kwa watoto wengi sasa kitu hiki kimekuwa ni lazima kwa mzazi kumnunulia.
Asilimia 26 ya watoto kati ya miaka 12 na 15 wanamiliki tablet computers,kiwango
kilichopanda kwa asilimia 7 ukilinganisha na mwaka jana.Takwimu zinatabiri kwamba kizazi kinachokuja kinakuwa cha kiteknolojia muda mfupi tu baada watoto kuacha kuvaa nepi,
hii ina maana watoto watajua teknolojia na kuitumia katika umri mdogo sana.Asilimia 28 ya watoto kati ya miaka miine na mitano hutumia tablet computers wakiwa nyumbani.

No comments :

Post a Comment