Oct 18, 2013

Inawezekana pengine Lenovo anataka nunua baadhi ya hisa toka BlackBerry.

Mtengeneza simu na kompyuta,kampuni ya Lenovo iliyoko China imehusishwa na ununuzi wa baadhi ya hisa kutoka kampuni ya BlackBerry.Hapo jana,makala ya Wall Street ilitaja kwamba Lenovo anaangalia uamuzi wake wa kununua hisa toka kwa BlackBerry,lakini kwa upande mwingine chanzo kingine cha habari cha Reuters kimesema Lenovo anataka chukua kipande kidogo tu cha kampuni na sio kampuni zima.


Kwa sasa kampuni hii ya Canada inahaha katika kurudisha heshima yake sokoni amabapo tumeona mabadiliko kutoka simu za keyboard ya qwerty iliyotengenezwa kwa plastiki mpaka simu yenye touchscreen kamili ikiwa na operating system mpya ijulikanayo kama BlackBerry 10 OS.

Tatizo linalotokea kwa Lenovo ni jinsi usalama wa mtandao wa BlackBerry ulivyo,hii itapelekea ugumu katika Lenovo kuweza kuinunua BlackBerry.Kwa hili,mpaka sasa ni swala linalompa sifa sana katika matumizi kiserikali na makampuni makubwa ya ushirika.Lakini pia kwa upande mwingine makampuni mengi yamehama kutoka katika mfumo wa BlackBerry na kuwa na mbadala wa iPhone na Android.Swala kama hili lishawahi kuikumba kampuni ya Huawei alipotaka kufanya biashara na Amerika ya Kaskazini.

Nchini Canada kuna sheria kwamba kama kampuni yoyote ya nje inataka kampuni kununua hisa ambazo inaonekana zinafikia kiwango kikubwa cha pesa basi ni lazima serikali iangalie kwanza kuna manufaa au kitu hicho kitahatarisha usalama wa nchi,kama ni manufaa basi serikali mpaka iidhinishe ndipo biashara ifanyike.

Lakini pia,sio kwamba  Lenovo akikamilisha dili hili atakuwa kaula,hapana.Ukiangalia sana soko la simu la kampuni hii liko ndani ya nchi yake ya China,kwa upande wa kompyuta ndipo ana wigo mpana wa soko.Anachojaribu kufanya katika soko la simu ni kutanua mbawa kimataifa zaidi,lakini si hicho hata nchini kwake bado anapata changamoto kutoka kwa kampuni kama Xiaomi ambayo inakuja juu sana.

No comments :

Post a Comment