Oct 24, 2013

Pamoja na misukosuko yote aliyonayo BlackBerry kwa sasa!lakini,kwa hili amefanikiwa.

Ni kitu ambacho kwa uhakika nadhani si Google wala Apple aliyewahi fanya.Pamoja BlackBerry kuwa katika kipindi kigumu lakini kafanikiwa kupenyeza kiasi kidogo lakini cha maana katika OS za Android na iOS,hapa ninaongelea app ya BBM ambayo imeanza onekana kwenye simu za Android zinazorun Android 4.0 na kuendelea na iOS zinazorun iOS 6 na kuendelea hapo jumatatu usiku.


Tangu kuachiwa kwa app hii kwenye Appstore,Samsung Apps na Playstore(katika baadhi ya nchi) ilifikia kiwango cha kuwa downloaded na watu milioni 20 ndani ya masaa 24 baada ya kuzinduliwa.Hii inaonesha ni jinsi gani watumiaji wengi wa Android na iOS waipendavyo BBM ila walianza tumia hizi OS nyingine kwa vitu baadhi tu,kama kucheza games na muonekano bora(User Interface),ila bado BBM itabaki kuwa ni social chatting app bora kuliko zote mpaka sasa.

 Kwa upande wangu,kilichonivutia sana ni jinsi muonekano wa hii app ulivyo ikiwa na muonekano sawasawa na BBM iliyopo kwenye simu za BlackBerry Z10 na Q10 ambazo zinatumia BB 10 OS.

 Ninadhani BBM itafanya vizuri sana kadiri siku ziendavyo,hii inaleta mchuano mkali sasa katika vita ya social apps ambapo tayari kuna apps nyingine zinazofanya vizuri sana katika Android na iOS ikiwamo Whatsapp na Viber.Katika hizi mbili watu hupendelea zaidi Whatsapp.

Kikwazo kimoja cha Whatsapp ni app ambayo inatakiwa lipia baada ya mwaka mmoja wa kuitumia bure katika Android  na vilevile katika iOS unatakiwa lipia kabla ya kuitumia.Tofauti kwa BBM,hii unapodownload iko tayari tumia mpaka uchoke.





No comments :

Post a Comment