Oct 2, 2013

LG wazindua display ya inchi 5.5 kwa ajili ya smartphones ya ubora mara nne zaidi ya kioo cha kawaida cha High Definition

Tumeona mabadiliko ya haraka katika smartphones kwa upande wa display zake hasa katika smartphones za gharama(high end smartphones),ilianza kwa Retina display(zinatumika hasa kwenye iPad) baada ya hapo HD display na sasa tuna Full HD displays.Pengine unaweza kuona hatuhitaji display zenye ubora zaidi ya hizi maana hizi ni bora haswa,lakini mashindano ya watengeneza vifaa hivi kwao ni kama kumekucha.


LG wametangaza display mpya yenye resolution ya 2560×1440 na pixel density 538ppi na kampuni hii wameipa jina display hii kama "Quad HD" ikimaanisha ubora mara nne wa High Definition,ambapo simu kama Samsung Galaxy S4 ina pixel density ya 441na Sony Xperia Z ikiwa pixel density hiyohiyo kama ya S4.Hizo ni baadhi ya simu zilizo na kiwango cha juu kwa sasa na unaweza kuona ni jinsi gani display zake zimeachwa mbali na hii display mpya ...
ya LG.

 LG bado hawajatangaza kioo hiki kitawekwa katika simu ipi mpaka sasa,ninadhani tutakiona katika moja simu za LG mwishoni mwa mwaka huu au baadaye mwakani,hii ni hatua kubwa kiteknolojia.

No comments :

Post a Comment