Sep 14, 2013

Nokia alijaribu Android OS katika simu zake kabla ya kupata dili kutoka kwa Microsoft.

Tunajua kwamba kwa sasa Nokia anatumia Operating System ya Windows Phone OS ambayo inamilikiwa na Microsoft.Lakini,kumbe wala haikutakiwa kuwa hivi.


 Ripoti ya New York Times imemulika ni vipi Nokia ingeonekana siku zijazo bila Microsoft ndani yake.Inadaiwa kwamba Nokia alikuwa akiijaribu Android katika simu zake za Lumia kabla ya kuingia mkataba na Microsoft.

 Nokia ana uwezo wa kuhamia kwenye Android mwishoni mwa mwaka 2014.Wahandisi wa Nokia wanadai ya kwamba ni rahisi sana kuweka Android katika Nokia Lumia zilizopo sasa hivi katika soko.


 Viongozi wakubwa wa Microsoft
walikuwa wanatambua kabisa kwamba kuna kampango cha chinichini cha Android ndani ya Nokia pamoja hiyo haikuwa ndani ya makubaliano yao.
Kuhamia kwa Nokia kwenye Android kutaiumiza sana Microsoft,watapata pigo kubwa sana.Ikiwa kwamba Nokia ana asilimia 80% ya Windows Phone zote zinazouzwa.Kwa upande mwingine itawasaidia Nokia,kwa sasa wanashikilia asilimia 3% katika soko ikiwa wameshuka asilimia 32.8% ukilinganisha na mwaka 2010.


 Nadhani mwakani tutajua vizuri kama Nokia atahamia Android au la...sijui itaonekana vipi!!!!!!


No comments :

Post a Comment