Sep 3, 2013

Mafanikio na kufeli kwa smartphones za Windows,chini ya uongozi wa Steven Ballmer.


Operating System ya Microsoft ya Windows Phone haina ushawishi mkubwa katika soko kama ilivyo operating system ya Windows katika desktop na PC.Wakati huu ambapo mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Microsoft Bwana Steven Ballmer akiwa ametangaza kustaafu hapo mwakani,tunaweza kumnyooshea vidole kwa kushindwa kuleta mafanikio hasa katika upande wa smartphones.

Lakini si kweli kwamba anahitaji kulaumiwa na kuonekana ni mtu ambaye kazi hiyo imemshinda.Tukirudisha kumbukumbu zetu hadi mwaka 2000 ambapo kampuni ya Microsoft ilikuwa ikijiandaa kuingia katika soko la simu ambapo ilizinduliwa Pocket PC 2002,hii ndiyo software ya kwanza kabisa katika version za software za simu za Microsoft.

Kwa miaka kadhaa kabla ya kampuni ya Apple haijazindua simu za iPhone,Windows Mobile zilikuwa zimeteka soko la smartphones,enzi hizo ambapo smartphones zilikuwa zikionekana moja ya kitu cha kitu starehe(luxury) kwa wafanyabiashara wakubwa ambao waliona kifaa ambacho ni rahisi kubebwa.

 Hapa ndipo kampuni ya Microsoft ikapata mafanikio makubwa sana na kuwa na hisa nyingi sana katika soko hasa nchini Marekani.Hisa zao zilifikia hadi asilimia 60% kwa mwaka 2007,pia huu ndio mwaka ambapo iPhone ilizinduliwa.

Baada ya iPhone kuzinduliwa,Microsoft kama ilivyo kwa Nokia na
BlackBerry walikuwa taratibu kuendana na changamoto ya uzinduzi wa iPhone katika soko! na hili ndilo kosa kubwa walilofanya.Tofauti na smartphones nyingine zote zilizokuwepo kabla ya 2007,iPhone ilivuta macho ya wengi kwa kuwa na Touchscreen bila keyboard!

 Google akiwa na Operating System ya Android,akawa ni mbadala wa  iPhone,kwa hiyo macho ya watu wote yakabaki kukodolea iPhone na Android,enzi hizo Android simu yake ya kwanza ikiwa Htc G1.

Microsoft alichukua muda sana kuweza kuendana na mabadiliko.Akaja na Operating System ya Windows Phone 7 ambayo ilikuwa ni full touchscreen,ikiwa na nia ya kupambana na iPhone na Android.

Mwaka 2011,Nokia alitangaza ubia na Microsoft,ambapo Nokia walikubali kutengeneza simu nyingi zilizo na Operating System ya Windows Phone.Hapo ndipo tukaanza kuona simu za Nokia Lumia.Lakini,wakati Nokia Lumia zikivutia watu baadhi ya sehemu za ulimwengu,hazijafanya lolote kubwa kwa kampuni ya Microsoft.Windows Phone OS inachukua asilimia 3.7% kidunia,ikiwa nyuma sana ya Android ambao wana asilimia 79.3% na iOS ikiwa na asilimia 13.2%.

 Pamoja na hayo yote,muda huu ambapo Bwana Ballmer anakaribia kuiacha Microsoft,atajuta sana kwa kauli yake ambayo si watu wengi walishawahi kumsikia akisema,alisema katika mahojiano na CNBC mwezi januari mwaka 2007,katika kuonesha msimamo wake kwa iPhone.

Alisema"Hiyo ni simu ya gharama sana duniani na haifai kwa wateja ambao wanategemea smartphones kwa biashara,haina keyboard na hii inaifanya isiwe bora katika kutuma barua pepe(emails)".Akaongeza kusema "Nimeangalia na kuona,mkakati wetu ni bora zaidi,naupenda sana"

 Si mbaya sana,kila mtu kuna muda anateleza katika maamuzi.Ari mradi kaleta mabadiliko makubwa kwa kampuni ya Bwana William Gates,Microsoft katika upande PC na Laptops,si mbaya sana!

No comments :

Post a Comment