Aug 18, 2013

Nokia anatakiwa kuanza kutumia Android kabla mambo hayajabadilika.

 Katika miaka ya nyuma hasa kuanzia mwaka 1998 hadi 2007,Nokia ndiye alikuwa mfalme katika soko la smartphones akiwepo na makampuni mengine kama RIM ambao sasa wanajulikana kama BlackBerry,Palm ambao walikuwa wakitengeneza smartphones zenye OS ya Web OS na Microsoft wakitumia Operating System ya Windows Mobile.


Mwaka 2007 ndipo smartphone ya kwanza ya Android ilizinduliwa Htc akiwa wa kwanza kutumia Operating System hii katika simu zake ambapo kabla ya hapo alikuwa akitumia Operating System ya Windows Mobile.Android OS ilivuta makini ya watu wengi sana ambao wengi wao walikuwa ni watumiaji wakubwa wa Symbian OS ambayo ni Operating System iliyokuwa ikitumika na Nokia,na wengine kutoka katika Operating System za Web OS,BlackBerry OS na Windows Mobile.

Nokia ndiye alikuwa kiongozi kwa kushika soko miaka yote hii kuanzia mwaka 1998 hadi 2007 ambapo ni takribani muongo mmoja,wale waliokuwa watumiaji wa Symbian OS ndiyo wakawa wateja wa simu zinazotumia Android OS ikiwa na Android version ya kwanza ikiitwa Android 1.5(Cupcake).

 Kampuni hii ya Finland ikaanza kupoteza hisa zake katika soko taratibu kadiri miaka inavyoenda,hapa ndiyo ukawa mwanzo wa Symbian kupoteza umaarufu wake,Nokia akaanza kuhaha jinsi gani ataweza kurudi katika soko zamani.Mwaka 2010 mazungumzo ya ubia yakaanza kati ya Nokia na Microsoft.

Baada ya mazungumzo hayo ya awali mwaka mmoja ukapita ndipo Operating System mpya iitwayo Windows Phone 7 ikazinduliwa hii ikiwa ni kazi ya pamoja kati ya Nokia na Microsoft,pamoja na hapo zilizinduliwa simu kama Nokia Lumia 710 na Nokia Lumia 800
zikitumia Operating System hii.

 Hadi mwaka huu mwanzoni tuliona hisa za Nokia zikirudi kwa kiasi fulani,japo si kiasi cha kutisha.Simu hizi zilivuta wengi katika nchi ya Marekani na baadhi ya nchi barani Ulaya,mvuto huu ulikuja baada ya kuboresha Operating System ya Windows Phone 7 na kuleta Operating System nyingine ya Windows Phone 8 ikiwepo katika simu kama Nokia Lumia 920,Lumia 820 na nyinginezo.

 Kuna umuhimu mkubwa wa kampuni hii kuangalia tena maamuzi yake na kuhamia katika mfumo wa Android,kampuni kama Htc kabla ya kutumia Android OS ilikuwa ikitumia Windows Mobile OS ambapo nayo ilihamia kwenye Android na kupata mafanikio makubwa sana.Pamoja na ya kwamba kwa sasa Htc ana baadhi ya simu zinazotumia Windows Phone 8 kama Htc 8x ila ni wazi kabisa simu hizi hazijaipa faida na mafanikio yoyote ya maana kampuni ya Htc ambayo ni ya Taiwan huko nchini China.
 Hisa za Nokia zimeanguka kwa asilimia 2.6%,mwanatakwimu mmoja alishawahi kusema "Nokia wanatakiwa kumeza kidonge cha Android kabla haijafika muda ambapo watashindwa fanya chochote".

Kwa sasa Nokia anakabiliwa na changamoto mbili.Kwanza,kuanza kupotea kwa simu za kawaida(features phones) na watu wengi kuanza kutumia smartphones ambazo nyingi zinatumia Android OS.Pili,kukosa mvuto kwa simu za Windows Phone kwa watu wengi.Hivi vitu vitaigharimu sana Nokia siku za mbeleni kwa kadiri mambo yanavyozidi kubadilika,wataalamu wengi wa mambo ya teknolojia wanatabiri kwamba baada ya miaka michache kama Nokia hatobadilika basi itakuwa ni kampuni mfu.

 Pamoja na Nokia kuzindua simu nyingine inayotumia Windows Phone 8 iitwayo Nokia Lumia 1020 yenye megapixels 41 za kamera lakini bado hiki si kitu kipya katika soko maana tayari tushaona kuna Samsung Galaxy S4 Zoom yenye megapixels 16 na pia kuna Sony Xperia i1 Honami itayokuwa na megapixels 20.

 Nokia anatakiwa kukubali matokeo na kuhamia Android OS.Je,unadhani ni sawa Nokia kufanya hivyo?

1 comment :

  1. Yes they should do move to Android. But it's getting rather late to do anything. Shame. Lol at the mortal kombat reference.

    ReplyDelete