Aug 14, 2013

BlackBerry 9720 yatangazwa na BlackBerry,ina qwerty keyboard lakini muundo ni uleule kama ea zamani.

Hii sasa nadhani ni maji kuzidiwa unga kama waswahili wasemavyo.Siku chache zilizopita BlackBerry ambayo zamani ilikuwa ikijulikana kama RIM wametangaza aina mpya ya simu iitwayo Blackberry 9720,simu hii ina keyboard aina ya qwerty na kioo chenye inchi 2.8.Cha ajabu ni kwamba simu hii inatumia operating system ya BlackBerry OS 7.1 ambayo kwa sasa inapitwa na wakati kama Operating system za Symbian na Windows Phone 7.

Kwa sasa BlackBerry wana operating system yao iitwayo BlackBerry 10 na ukiangalia simu hii iko na kiwango cha chini katika hardware mpaka software,hii ni wazi kwamba simu hii ni mabaki ya modeli za nyuma ambapo iliachwa katika uzinduzi wake na sio kweli kwamba ni simu mpya kulingana na muda wenyewe.

Simu hii ni mahususi kwa watu wanaohama kutoka katika simu za kawaida na kutaka kutumia smartphone za gharama nafuu,imelenga zaidi Asia,Afrika,Ulaya na Latin Amerika.

No comments :

Post a Comment