Jul 22, 2013

Kauli ya Huawei kwa Marekani:"Fungeni midomo au wekeni mambo sawa"

Huawei amejibu tuhuma dhidi yake zilizosemwa na serikali za Marekani na Uingereza kwamba anachunguza nchi hizo mbili na kupeleka taarifa kwa serikali yake ya China.
 Katika kujibu tuhuma za hivi karibuni zilizosemwa na serikali za Uingereza na Marekani,kampuni ya vifaa vya mawasiliano ya Huawei ambayo ni ya nchini China imetoa kauli kali dhidi ya tuhuma hizo.

 Makamu rais wa mahusiano ya nje wa kampuni hiyo Bwana William Plummer amezitaka serikali hizo mbili kufunga midomo yao kama wanashindwa kutoa ushahidi wa kutosha wa kubeba tuhuma hizo kwamba kampuni hiyo inazichunguza serikali hizi mbili kwa niaba ya serikali ya nchi ya China.

 Bwana Plummer alikuwa akiongelea kauli toka kwa kiongozi mstaafu wa CIA Bwana Michael Hayden kwa kusema kwamba Huawei inatoa taarifa kwa serikali ya China.Katika mahojiano na gazeti la Australian Financial Review lililochapishwa alhamisi ya wiki iliyopita alisema kampuni hiyo imetoa maarifa iliyopata wakati ikifanya kazi za kimawasiliano na kampuni za Kimarekani na za Kiingereza kwa serikali yake ya China.


 "Ni muda wa kufunga mdomo au kuweka mambo sawa"alisema kiongozi mmojawapo wa kampuni ya Huawei.










No comments :

Post a Comment