Jul 22, 2013

Umiliki wa Smartphones Korea ya Kusini waongeza mara tatu zaidi katika kipindi cha miaka miwili,Inaongoza duniani.

Takwimu za hivi karibuni zinaonyesha kwamba Korea ya Kusini imeendelea kuongoza katika kuwa na namba ya watu wengi wanaomiliki Smartphones kuliko nchi yoyote duniani,ikiwa na asilimia 73% ya watu wanaomiliki simu hizo.Kiasi hiki kinakaribia sana kuwa mara tatu zaidi ya takwimu za mwaka 2011.

 Hii ni mwaka wa pili mfululizo nchi hii inaongoza katika hii sekta,ambapo kwa mwaka jana tu kulikuwa na asilimia 67.6% ya watu wanaomiliki Smartphones katika nchi hiyo.Inavutia sana ambapo kwa wastani wa kidunia ni asilimia 14.8% tu na hata masoko mazuri ya ununuzi wa Smartphones kama Marekani yapo katika ukaribu wa asilimia 50% tu.

Pamoja na kuonyesha ukuaji huu wa hali ya juu,asilimia 72% hutumia kwa ajili kuperuzi katika mtandao na asilimia 43% hutumia katika kuangalia video.


Ukuaji mkubwa katika hii sekta unapewa msukumo mkubwa sana kutokana na kufanya vizuri kwa makampuni ya kutengeneza vifaa vya kielectroniki ambayo ni Samsung na LG,ambayo yote ni ya Korea Kusini.Yameleta msukumo mkubwa sana wa ukuaji wa kiuchumi na kusaidia sana ukuaji wa Sayansi na Tekonolojia katika nchi hiyo.

No comments :

Post a Comment