Jul 2, 2013

Picha inayodaiwa kuwa iPhone ya gharama nafuu yaonekana mitandaoni.

Kava ya nyuma ya simu ambayo inadaiwa ya kwamba itakuwa ni iPhone ya bei nafuu imevuja mtandaoni.
 Picha hizi zinaonesha muonekano wa housing ya simu hizi zikiwa katika rangi tofauti tofauti.Hii inakuja baada ya uvumi uliokuwepo wiki chache zilizopita kwamba kutakuja na simu ya iPhone ya bei nafuu.

Haishangazi sana kuona picha hizi za housing ya inayodaiwa itakuwa ni iPhone ya bei ya chini.Kwa nyuma inaonekana kuna camera ikiwa na single LED flash na pia kuna microphone ya nyuma ambayo ipo katikati ya camera na single LED flash.Kama kawaida logo ya Apple ipo kwa juu kidogo ya simu ikiwa ni ileile inayotumika katika simu za iPhone zilizopo.Kwa chini kuna neno lililoandikwa iPhone.


Chanzo cha picha hii ni kutoka mtandao uitwao micro-blogger,mtandao huu una uhusiano mkubwa sana na wafanyakazi wanaofanya kazi katika viwanda vya simu China.Picha hizi zinadaiwa zimepigwa katika kiwanda cha Foxconn ambacho ndio hutengeneza simu za iPhone na bidhaa zote za Apple,kompyuta za HP,Xbox na bidhaa nyingine nyingi za kielectroniki.

Hizi ni tetesi tu hamna taarifa yoyote rasmi,nadhani katika wiki nchache tetesi hizi zitawezwa thibitishwa kama  ni kweli au la.


No comments :

Post a Comment