Jun 17, 2013

Album mpya ya Jay Z iitwayo Magna Carta Holy Grail itapatikana bure kwa mamilioni ya watumiaji wa simu za Samsung Galaxy.



Mamilioni ya watumiaji wa simu za Samsung Galaxy watapata albamu ya Jay Z katika simu zao siku tatu za mwanzo bure.

Samsung wameamua kushiriki katika albamu mpya ya msanii wa Hip-Hop wa Marekani Shawn Carter au kwa jina la kisanii Jay Z kwa kuitoa bure albamu yake yenye jina "Magna Carta Holy Grail".Albamu hii itapatikana kwa wale wanaomiliki simu za Galaxy modeli ya S3,S4 na Note 2 ambapo watatakiwa kwanza kudownload application maalumu.

Application hiyo ambayo itaanza kuwa downloaded kuanzia tarehe 24 mwezi huu itaelezea undani wa albamu hiyo katika kuitayarisha na tarehe 4 mwezi wa saba ndipo albamu hiyo itapatikana ambapo itakuwa ni siku tatu kabla ya simu ambazo sio Galaxy S3,S4, na Note 2 nazo kuweza kupata albamu hiyo kwa malipo.

Ubia kati ya Samsung na Jay Z ambao wote wawili ni wwatafuta masoko sana katika biashara zao ulionekana mara ya kwanza katika tangazo lilioneshwa katika televisioni kubwa kwenye fainali za NBA.

Jarida la Wall Street limeripoti kwamba Samsung wamelipa $5 za kimarekani kwa kila copy kwa mamilioni ya copy za albamu,pengine wataifanya album kuingia platinum wiki chache kabla ya kuzinduliwa rasmi.

 Makampuni mengi ya Korea ya Kusini ya kutengeneza simu yameona kuna faida kulipa ili kupata uaminifu katika nchi ya Marekani kutokana na ushindani wake na kampuni ya Apple katika kugombania hisa za soko katika biashara.

1 comment :

  1. EDWARD MWALYEGO3:40 PM GMT+3

    t man hii blog ya ukweli knoma! hongera

    ReplyDelete