May 15, 2013

Samsung imesafirisha Samsung galaxy s4 milioni sita,yavunja rekodi yake iliyopita

Hakukuwa na shaka kabisa kwamba Samsung galaxy s4 itakuwa ni simu yenye mafanikio makubwa katika soko la simu,swali lilibaki,je!itaweza kuvunja rekodi iliyoweka nyuma ya simu zake zilizopita kama samsung galaxy s3 na galaxy note 2? Kampuni hii ya Kikorea imeweza kusafirisha zaidi ya simu milioni sita aina ya galaxy s4 ambayo ndo flagship smartphone ya kampuni hii kwa sasa hadi ijumaa iliyopita ikiwa ni wiki mbili toka simu hii iingie sokoni.Lakini mauzo ya juu yalitokea siku nne za mwanzo ambapo ziliuzwa simu zipatazo milioni nne. S4 inaweza kuwa na mwendo ule ule wa kufanya vizuri toka iingie sokoni,watengenezaji hawa wanaweza kufikia malengo yao ya kuuza simu milioni kumi ndani ya mwezi mmoja toka kuzinduliwa kwake.Ukiangalia flagship za nyuma kama samsung galaxy s3 ilichukua siku 21 kufikia mauzo ya simu milioni tatu wakati samsung galaxy s2 ilichukua siku 55,galaxy s ilichukua siku 85 kufikia mauzo ya simu milioni tatu. Pamoja na mchuano mkali Samsung inayopata kutoka kwa simu wenzake za makampuni mengine kama HTC One na Sony Xperia Z ambazo nazo hazina muda mrefu toka kuingia kwake sokoni bado inauza vizuri sana karibu mara kumi ya flagship zake zilizopita kama galaxy s2 na s3.

No comments :

Post a Comment