May 15, 2013

Instagram inakuja siku za karibuni katika windows phone,imeonekana katika page ya twitter @instagramWP

Huenda wewe ni mmoja wa watumiaji wa windows phone kama nokia lumia,htc au yoyote ile inayotumia windows phone operating system ila unasikitishwa na kukosa official application ya Instagram huenda hii ikawa habari njema kwako. Leo Nokia wametangaza app yao mpya ikiwa ni ushirikiano na hipastamic ambayo unaweza share picha katika mtandao wa instagram.Lakini cha kushangaza,account yenye jina @instagramwp imeonekana katika mtandao wa twitter ikidai kwamba ni ukurasa rasmi wa instagram kwa windows phone,katika kuangalia nokia ndo alikuwa wa kwanza kufollow hiyo page,hii ikiondoa mashaka kwamba ni wazi application rasmi ya Instagram kwa wimdows phone iko njiani. Kwa wale mnaofatilia Nokia amekuwa na shauku kubwa sana ya kuleta instagram katika simu zake za lumia,sasa tusubiri tuone hiyo Instagram katika simu za windows phone,

No comments :

Post a Comment