May 17, 2013

Nexus 4 nyeupe ikiwa na Android 4.3 inakuja mwezi ujao tarehe kumi

Mwaka huu hatujaona version mpya ya Android katika mkutano wa Google I/O ambao unaisha leo,kulikuwa na maboresho makubwa katika application za Google maps,Google+ na Hangouts.Kuboresha zaidi Google play music na huduma mpya ya Google inayohusiana na games.

 Mkutano huu ulilenga sana kuonyesha maendeleo kwa developers ambayo hayahitaji version mpya ya android inayokuja.Hata hivyo android 4.3 itaitwa Jelly Bean au Key Pie Lime,bado taarifa ya jina lipi kutumika hasa hazijathibitishwa.

Hiyo ndo LG Nexus 4 ambayo itatoka na ikiwa na Android 4.3,tusubiri tuone Google ataleta maboresho na mabadiliko gani katika operating system hii,ili kuweza kuwapiku wapinzani wake kama Apple na Windows phone ikiwa pia na BlaclBerry anakuja juu kwa kiasi kikubwa na oerating system yake ya BlackBerry 10 iliyo na utofauti mkubwa na simu zake za nyuma.

No comments :

Post a Comment